Friday, December 4, 2009

Nakaribisha mawazo juu ya kuweka jiji letu na hatimae nchi yetu kuwa na mazingira mazuri na masafi.

Karibu utoe ushauri, mawazo, kuhusu mada yetu ya kutaka kuanzisha kuweka jiji la Dar na hatimae Tanzania kuwa na mazingira mazuri na usafi kwa ujumla.

Sylvia-Director

2 comments:

  1. Mh, mi nadhani ni wazo zuri but Watanzania inabidi tubadilike kwanza , kutupa tupa uchafu ovyo tuache,pia serikali isaidie kuweka dustbins sehemu mbalimbali,mi nipo nje ya Tz yaani huwezi ona mtu katupa eti chupa ya maji( baada ya kumaliza kunywa) kuna dustbins almost every where,na ukionekana ni fine.Labda hiyo nayo ianze hapo,jiji liweke dastbins then fines zitawale labda tutabadilika. Vinginevyo itakuwa ngumu km hatutabadili tabia ya kuchukia uchafu

    ReplyDelete
  2. Mi nadhani japo hili ni jukumu la kila anayeishi Dar, lakini kwa kiasi kikubwa linaweza likafanikiwa kama serikali za mitaa wakisimamia na kuongoza shughuli hii. Kuna mji niliwahi kuishi, ilikuwa kila Jumamosi asubuhi watu wa serikali za mitaa na maafisa afya wanapita kukagua na kusimamia shughuli za usafi. Ilisaidia sana kwani ilikuwa wakikuta eneo ni chafu basi wote mnaoishi pale mnawajibishwa kwa kulipia fidia na kupasafisha pia. Nimeshangaa sana kuona hapo Mwenge tu kwenye barabara mpya inayotoka ubungo unakuta katikati ya barabara ambapo kumepandwa mimea/ mau mazuri laikini pamegeuza jalala na watu wanazidi kuongeza takataka kila siku. Naamini maeneo yale kuna viongozi wa mitaa na maafisa wa afya. Ifanyike juhudi za makusudi ili kuwe na chombo kitakachokuwa kinasimamia wananchi kusafisha maeneo yao.

    ReplyDelete