Thursday, October 10, 2013

KABATI ZA JIKONI KATIKA MUONEKANO WA 3D

Katika muendelezo wa ku design 3d upande wa jikoni.



Naomba niwafahamishe wadau wote kua, kabla ya kufanya design ni lazima tujue kua jiko hili litatumikaje? na eneo letu litatutosha?  kuna aina mbili hapa, kuna jiko ambalo tayari limesha jengwa, na kuna lingine ambalo bado halijajengwa.

Kwa hili ambalo limejengwa tunachokifanya ni kucheza na space iliyoko katika ku design........

Ambalo halijajengwa tutaanza maandalizi, na kidogo hii hua nirahisi zaidi, ambapo tunahitajika kujua ni watu wangapi watahitajika kuwepo katika jiko letu, na je watapishana vizuri, na je nafasi itahitajika kiasi gani kwa ajili ya makabati, jiko, sink, fridge etc....

Nakumbuka kipindi cha nyuma nilishawahi kuzungumzia aina za majiko, na utachagua jiko lako liweje kulingana na ukubwa wa eneo lako la kiwanja. na hata kama limesha jengwa basi itaaangaliwa ni design gani inaweza kufaa kwa jiko lako, na kama kutakua na marekebisho madogo madogo basi yatafanyika ili kuweza kuwekwa sawa.

Wednesday, October 9, 2013

MORE 3D DESIGN,

Tunaendelea ku design kwa 3d kwa wateja wetu........na hii husaidia kujua fanicha zikaeje, rangi ziweje, floor pia iweje,  mapazia ya rangi gani etc......

DAY BED....AVAILABLE BY ORDER @ HOMEZ DECO....(hardwood mkongo & mninga)

 Day bed hutumika kwa kupumzikia, unaweza kukiweka sitting room, balcony, ama kwenye korido kama ina nafasi......

Thursday, October 3, 2013

3D DESIGNS......



3d ni michoro ambayo huchorwa kwa kutumia computer na software maalum, ili kuweza kuona ni jinsi gani jengo lako itakua tayari baada ya kujengwa, na muonekano wake kwa ujumla, mpangilio wa fanicha ndani, na kuweza kukuonyesha makosa madogo na makubwa......

Hapa chini ni baadhi ya michoro ya 3d, ambapo tumeweza kuonyesha mfano wa nyumba itakavyoonekana baada ya kwisha kujengwa kwa nje....

3d yaweza kua niya garden, ya nyumba nje, ya mpangilio ndani, etc....ni wewe mwenyewe unahitaji nini.....


 Katika kazi yangu hii nimekua nikikutana na makosa mbali mbali ambayo wateja wangu wamekua wakiyalalamikia, kwamba jiko limekua ni dogo, ama chumba kidogo. ama hakutaka muelekeo huo.....mara vipimo havieleweki, rangi sio nzuri.......mpangilio wa fanicha. vitu haviendani. switch za umeme hazikuaa sehemu husika...etc.....ni tatizo kwa kweli......

Kitu kingine nimegundua kua katika ujenzi wa nyumba zetu, hua hatuna ule utaratibu wa kua wawazi kwa archtects(wachora ramani). Hausemi nini unataka, yaani we umeona nyumba ya flan basi unataka kua kama na yake na inabadilishwa kidogo tuuuu.......(copy and paste).

Jamni designs za nyumba ziko nyingi mno.....na ndio maana utakuta hapa kwetu nyumba zinafanana mno.......ukiona nyumba imebadilika basi ujue hiyo nyumba mwenye hakai sana hapa, kaja na mchoro wake toka nje.....

(nitalizungumzia hili siku ingine kwenye mada yake) inafika kipindi tuambizane ukweli....sasa......(let's be creative)

 kwa upande wa 3d, kama tungekua tunafuatilia ama kujua mapema, wengi wetu tusingekumbana na matatizo haya....maana saa ingine utakuta ukuta umezidi, inabidi kubomoa.......sasa hizo ni gharama zisizokua na maana.......

Tuesday, October 1, 2013

MAANDALIZI YA MWISHO WA MWAKA KATIKA NYUMBA ZETU.......

Wengi wetu tumekua na kawaida ya kujiandaa kwa ajili ya mwisho wa mwaka, kama kwenye maofisi basi tunapamba ofisi zetu kwa mapambo, na kama ni kwenye nyumba zetu basi nako tunajiandaa kufanya maandalizi.

Asilimia kubwa kati yetu ni kua hua katika kipindi hiki hua tunajitahidi kumalizia nyumba tunazojenga ili tunahamia, na wengine tunahamia kwenye nyumba zengine za kupanga....kubadilisha mazingira....etc.

Katika yote haya maandalizi yanahitajika.......na inategemea pia na nyumba yenyewe inahitaji nini.....

Kwenye upande wa matengenezo, ama rangi, etc....

Bila kusahau pia fanicha, nazo pia inatubidi tuangalie, kama zinahitaji marekebisho, ama zinahitaji kubadilishwa kabisaaa.....yote haya yanaanzia kwako na wewe mwenyewe.

Katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ndio wengi wetu tanaangalia je yale malengo yetu tuliyoyapanga kwa mwaka mzima yamefanikiwa, ama yalikaribia kufanikiwa.

Napenda kukumbushia kua hiki ndio kipindi cha kufanya maandalizi ya nyumba zetu......kwa usafi, kutoa vitu ambavyo hauvihitaji na kugawa, na kama kuna vitu vibovu basi ndio wakati wake wa kuviteketeza.....

Pale ambapo unapopanga mikakati yako ya kimaendeleo, tusisahau na nyumba zetu.....

Jamani nyumba nazo zinahitaji service.....yaweza kua ni ya kila mwaka, ama ya baada ya miaka kadhaaa....ni wewe mwenyewe ndio utaangalia nyumba yako iko katika hali gani.....

Tumekua tukijisahau sana kwa upande wa kufanyia service nyumba zetu.......na mwisho wa siku unakuja kukuta matengenezo yanakua ni gharama zaidi ya matarajio yako..........wakati ungekua unafanya service ungeepuka tatizo hili la gharama mara dufu......