Wednesday, January 30, 2013

Taa za urembo ....


 Hizi ni taa za urembo, ambazo hutumika sebuleni,ama vyumbani. ila pia hutokana na ukubwa wake.....Taa hizi huvutia sana na zinaleta ladha uzitumiapo......Hufanya chumba kua na mwangaza na hupendezesha chumba....


 Taa hizi ziko za aina tofauti, na kulingana na matumizi yako......

Tuesday, January 29, 2013

Homez Deco sasa ni wakala halali wa Dulux Paints...... Homez Deco inayo furaha kuwafahamisha kwamba, tumechaguliwa kua wakala wa Dulux Paints....Nianwashukuru sana wadau wangu wote, kwani mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ninyi.....

Hizi ni rangi za ndani, na  nje... ambazo zina ubora wa hali ya juu, na pia zimetengenezwa mahususi, kwa kubana matumizi mengi ya rangi...nikiwa na maana ya kwamba, mahali pa kutumia ndoo 5 wewe utatumia ndoo 3.Utumiapo rangi hizi, matumizi yake ni madogo, na zina ubora wa hali ya juu, kwa upande wa finnishing, na zina ubora wa miaka 8 tokea umepaka ukutani, Hazi pauki, hazi fifii.....

Hapo juu ni baadhi ya rangi za dulux zilizotumika kwenye baadhi ya vyumba.....

Curtain Designs.....


 Design hizi zote zinapatikana Homez Deco, Hizi  ni design za curtain box.

Metal Beds available @ Homez Deco by order....

 Price, size 5 by 6 Tshs. 350,000/-
  Price, size 5 by 6 Tshs. 380,000/-
  Price, size 5 by 6 Tshs. 390,000/-

Sunday, January 27, 2013

Rangi zanye giza......

 Kumekua na tatizo la wengi wetu kupenda rangi zenye giza...ama Dark colors, kwenye nyumba zetu, ama maofisini kwetu....Rangi hizi zinahitaji sana mwanga, nikisema mwanga ni kuanzia mwanga wa asili, na pia mwanga wa taa wakati wa usiku.......Rangi hizi hufanya chumba kua kidogo na chenye giza.....haijalishi umezitumia wapi...maana kokote unaweza kutumia ila zitumike kwa mpangilio kama unapenda rangi zaidi ya moja.

Metal Double Decker Beds, Designs, Available @ Homez Deco.....by order

 Price, size 4 by 6 Tshs. 600,000/-
 Price, size 5 by 6 below, up 4 by 6 Tshs. 750,000/-

Price, size 5 by 6 below, up 4 by 6 Tshs. 750,000/-

Wednesday, January 23, 2013

Dustbin za jikoni..... Dustbin za jikoni mara nyingi hua zinasahaulika sana kusafishwa, na kama zikisafishwa basi hua hazitakati, na sabuni zinazotumika kusafishia, zinatakiwa ziwe zinaua vijidudu.....
 Haijalishi ni dustbin ya design gani unayo ama ni kubwa ma ndogo inategemea na matumizi yako.....Dustbin zinatakiwa zisafishwe kila siku, kama sio mara mbili kwa siku basi hata maramoja kwa siku......
Dustbin ziko za aina nyingi, niwewe tu unahitajika kununua kulingana na matumizi yako......

Tuesday, January 22, 2013

Metal Beds designs......available @ homez deco by order.....

 Price size 5 by 6 Tshs. 350,000/-
 Price size 5 by 6 Tshs. 400,000/-
 Price size 5 by 6 Tshs. 350,000/-
 Price size 5 by 6 Tshs. 390,000/-
Price size 5 by 6 Tshs. 350,000/-

Huduma mpya kutoka Homez Deco.....

 Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kua Homez Deco imeanzisha huduma mpya ya kupasi mapazia kwa kutumia pasi ya mvuke, hii ni pasi ya mvuke, ambayo hainguzi, na mapazia yatapigwa pasi yakiwa tayari yameshatundikwa dirishani, iwe ni poles, curtain box etc....
Mapazia yatapigwa pasi na sisi, kwa kutumia pasi hii, pazia zako inaweza zikawa zimetoka kufuliwa, ama ni mpya, na haijalishi umenunua wapi.....yote tutapiga pasi....Tutakuja nyumbani kwako, ama ofisini kwako kuja kukupa huduma hii....

Kwa dirisha moja tutacharge 15,000/- usafiri ni juu ya mteja......


Karibuni kwa huduma hii mpya kutoka kwetu....


Wasiliana nasi kwa namba 0713 - 920565 ama email address: sylvianamoyo@yahoo.com

Monday, January 21, 2013

Unahifadhi wapi products zako za bafuni, bafuni kwako? Hizi ni baadhi ya design za mabafu, ambapo zinatuelekeza ni vipi tuweze kuhifadhi products zetu kwa usalama na usafi zaidi....na katika mpangilio mzuri... hakikisha pia bafuni kuna kaa pakavu muda wote, nirahisi mno, mtu anaenda kuoga ahakikishe anakausha maji, kuanzia ukutani, mpaka chini. hii itasaidia sana kuhakikisha kua panakaa pakavu..

Friday, January 18, 2013

Color combo......Nyumba hii iko kunduchi, na nilipenda mpangilio wake.....

 Sitting room ni nzuri, simple, etc.....Fanicha zote hizi za mbao zimetengenezwa hapa hapa Tanzania-Dar...
 Hapo juu ni sitting room, umeona hiki kiti kilivyo na design kama ya kusuka vile......Angalia pia rangi zake alizo tumia, hua nasema, ukijiamini kwenye rangi kila kitu kitakua sawa...na ukiwa umekwama mahali, basi tuwasiliana.....Mdau huyu rangi alizozitumia ni white, orange, green, blue, na brown ambayo ndio viti vyake...
Rangi hizi ukiangalia picha hizi kwa makini, utaona kua kuwenye hii cusion ya green ina colors zote, kasoro brown.....Siku zote kwenye upande wa ku design, angalia vitambaa vyako vya sofa, ama pazia je vina rangi nyingi? kama ndio, basi tumia rangi hizo kwa kuendeleza kupamba nyumba yako na hii itakusaidia, kuto kuchanganya rangi, ama kua na rangi zaidi zisizoendana...
 Open Kitchen.....Ukiangalia hii dinning table, huoni hata muungo mmoja wa kati ya mbao na mbao....utadhani furniture hizi zimeagizwa nje ya nchi vile....kumbe ni kazi ya mtanzania mwenzetu...

Thursday, January 17, 2013

Duka jipya la vyombo.....Duka liko Kinondoni
Karibuni TerryTevi's Kitchenware,.

Hii ni kazi ya Homez Deco, Tulipaka rangi, na tukatengeneza hizi shelves za chuma, na kupanga vyombo kwenye duka hili....

Duka hili liko kinondoni, ukifika kinondoni mwembeni/makaburini kama unatokea mjini unaingia bara bara ya  kulia ni ya vumbi, na maduka yako baada ya garage kulia kwako....ni duka no. 5

Kwa mahitaji yako ya vyombo, wasiliana na 0715 - 350912

Karibuni....

Tuesday, January 15, 2013

Design za vitanda.....kiti/kitandaHii ni design ya vitanda na ni vile vile kiti.

Simple bathroom
Hili bafu ni dogo, lakini jinsi lilivyo pangwa kwa mpangilio....linapendeza.....Ninachoweza kusema ni kua, kwa wewe ulie na sehemu ndogo, nikiwa na maana bafu ni dogo, usilidharau. Liweke katika mpangilio mzuri na usijaze mavitu, ukifikiri kua ndio kulipamba ama kuliweka vizuri.

Monday, January 14, 2013

Color of the year 2013- Emerald GreenHizi ni baadhi ya design kwa kutumia rangi ya mwaka 2013.....rangi hii inaweza kutumika chumba chochote kile, na unaweza pia ukaipunguza makali, nikiwa na maana ya kua unaweza kutumia dark color ama light color, kwenye ukuta, sofa, carpet, decorations etc....