Wednesday, August 3, 2011

Mapazia - Mbezi
Hizi ni picha ya mapazia tuliyoshona site ya mbezi kwa mteja. Namshukuru mteja wangu huyu, kwani alikubali tupige picha na tuweze ku share picha hizi.

Nyumba bado ni mpya, sasa yeye anatengeneza nyumba yake kwa awamu, si mnajua kila kitu kinawezekana? Haijalishi una hela ama hauna.

Amejenga nyumba yake, umekwisha aakaahamia, akaanza kutengeneza pazia, halafu ndio fanicha. etc

Hapa tuko kazini, busy,, kwa kweli Homez deco haijalishi bosi ama mfanyakazi, wote tunaingia mzigoni ili ku meet deadline, na kazi iweze kuwa nzuri, (umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu).

(fuatilia picha zaidi, wakati tunakwenda kumfungia nyumbani kwake)Stay tunned

Ukimya wangu


Habari za masiku wadau wangu,

Poleni sana kwa kuwa kimya, mambo yaliingiliana, (kifamilia). Ila ninamshukuru Mungu sasa niko poa na ninaendelea vizuri na ujenzi wa taifa.

Niliwa miss sana sana sana.

Tuko wote, sasa.

From,
Sylvia Namoyo.aka Mama Jaydan
Director