Monday, December 21, 2009

Kazi ya jumapili. Nilikwenda kumfungia mteja mapazia niliyomtengenezea. ASANTE MAMA CATHERINE WA MBEZI. Wewe wangoja nini?

Jumapili ya jana tarehe 20/12/09 nilikwenda mbezi ya kimara kwenda kumfungia mapazia mteja wangu Mama Catherine. kwa kweli nashukuru kazi yangu ameipenda. Aliniomba nim dizainie mapazia ya sitting room kwake na jikoni. Nikaenda kwake kuangalia anarangi gani na dizaini za furniture alizonazo. Sasa nilimchagulia matirio ya vitambaa na nikamuonyesha akapenda. Nika dizaini mwenyewe, na nimechagua dizaini hii ya mapazia kwa sababu makochi yake tayari yana urembo. Hivyo ningeweka urembo mwingine kwenye mapazia pasinge onekana. Guess what, X-MASS TREE AMEPAMBA MTOTO WAKE WA MIAKA 6 AMBAYE NDIE CATHERINE AKISAIDIWA NA DADA YAKE MLEZI. NILIUPENDA SANA MTI. NINACHOTAKA KUSEMA MTI WA X-MASS HAUNA FOMULA.
Mapazia haya ya kijani ni ya jikoni, nimeamua kuweka kijani kwa sababu kijani inaashiria uoto wa asili, vyakula etc. Kwa upande wa jikoni kama una rangi nyeupe ukutani weka pazia lenye rangi rangi ili kuongeza fleva jikoni na kupunguza ukali wa rangi nyeupe.
Picha za chini ni kabla sijaweka curtains

7 comments:

 1. Sebule yake imependeza sana. Hivi hizo holder za pembeni unachomelea au??

  Hilda

  ReplyDelete
 2. Nashukuru sana dada,

  hizo holder sijazichomelea, nina drill ukutani na kufunga na scrue, na ninaziba mashimo yote nitakayoyakuta ukutani ili kupendeze zaidi.

  ReplyDelete
 3. Hayo ndo mambo!! Mbona tutakoma tushindwe wenyewe tu. Hongera sana dear

  ReplyDelete
 4. Nimeipenda kazi yako, akika ww ni m bunifu unaejua nn unakifanya Big Up sis.

  Ima (The Designer)

  ReplyDelete