Thursday, December 10, 2009

Decorate your home in one day

Habari za sikukuu, leo nitazungumzia ku decorate nyumba yako ndani ya siku moja kwa gharama nafuu sanaaa na waweza kufanya wewe mwenyewe kwa msaada mdogo wa mafundi. Nianze na mapazia, fua pazia lako hilohilo ulilonalo kwa sasa ila ongeza fleva kwa kuweka kitambaa juu ya hilo pazia kama picha inavyoonekana hapa ila rangi zisipishane sanaa.
Kwa upande wa chumbani, tandika mashuka yako masafi sio lazima yakawa mapya inategemea na mfuko wako, ila ni vizuri zaidi yakawa yanafanana. tundika picha ukutani ambapo kitanda kimeegemea kama kwenye picha hapa na kama una chest droo basi weka ua juu yake, hakikisha taa zako zina mwanga wa kutosha, kama una bedside lamp na zile lamp shade zake zimechakaa basi badilisha nunulia mpya, kama una tiles weka carpet ndogo eneo unaloshukia wakati ukitoka kuamka, kama una carpet eneo lote basi lifanyie usafi na utakuwa umemaliza.

Mara nyingi vyoo vyetu huwa tumeweka tiles, na kumbuka kuwa kwenye ile mistari ya tiles huwa kuna kuwaga na ukungu, mwambie fundi akuwekee filler ni unga wa tiles na zitaonekana ni mpya. Kama hakuna tiles basi paka rangi, na malizia kwa kuweka ua, mshumaa na spray ama kuna balls za marashi mahsusi kwa chooni huwa zinasaidia kukata harufu ya choo.


Wow, karibu to the heart of the house. sasa hapa, paka makabati yako rangi, ongezea ua natural panga vyombo vyako kwa mpangilio mzuri, hakikisha taa inawaka vizuri, na mwanga wa jua unaingia vizuri na kuwe kusafi bila kusahau mapazia.



Lovely is it? Mara nyingi wengi wetu wanadhani kupaka rangi sitting room nzima ni fashion sasa kama huna hela na unataka pabadilike unafanyaje? Jibu ni hili, paka rangi ukuta wako unaokaa tv kwa rangi ambayo iko bright. Punguza makabati na mavitu mengi tuwekayo kwenye ukuta huo.
USIJARIBU, FANYA UNIPE JIBU.




6 comments:

  1. mambo vipi sasa mimi nayapenda sana hayo mashuka pamoja na hizo foronya zake na hiyo mito midogo na mikubwa napenda sana ila sijui bei yake na pamoja na sehemu ya kuvipata, naomba unisaidie

    Hilder

    ReplyDelete
  2. Hi Hilder,
    mambo poa namshukuru mungu kwa yote, sasa wee uko wapi? kuna mzigo wa mashuka umeingia ingawa sio mengi, sasa nitayapiga picha na utachagua, yako ni foronya mbili za mito mikubwa, duvet cover na shuka moja. na kuhusu mito nitakufanyia kazi hiyo ya kukutafutia nipe size tuuu.

    Bei pia nitawaambia.

    Asante sana Hilder na siku njema.

    ReplyDelete
  3. Sylvia between you and me kama vile bendera ya tz imekosewa kwenye total visitors, angalia ili kama ndivyo uirekebishe. Thanks

    ReplyDelete
  4. Thanks Emmy nilikuwa sijaiona hizi bendera huwezi zibadilisha ila nitatafuta yenye bendera yetu.

    ReplyDelete
  5. mambo sylvia

    mimi size ya mito yangu ni ile midogo ya kawaida ya summary ila ugonjwa wangu mkubwa ni hiyo mito mikubwa na midogo pamoja na hizo foronya na shuka zake yani napenda sana huo mchanganyiko wa rangi. usisahau kuni bei. mi nipo ilala

    Hilder

    ReplyDelete
  6. Mambo safi Dada Hilder,

    Usihofu nitakutaarifu mara tuu itakapokuwa tayari.

    Weekend njema

    ReplyDelete