Tuesday, December 8, 2009

Email kutoka kwa Mrs.Jossanne George (She is Tanzanian)from New York City-America

ABSOLUTELY, KTK MIJI MISAFI NI MOSHi, ARUSHA, MWANZA

Huwa na ninaithamini sana, hii, miji, ni wasafi mpaka nje ya nchi watalii wanajuwa hiyi miji.

Tatizo la mji wa DAR ni kuanzia ngazi za juu serikalini, baathi ya viongozi tuliokuwa nao hawana mapenzi ya dhati na kazi yao wala, mapenzi na.mji ni viongozi wachache sana, wenye kujali na kuguswa na hili suala la mazingira mzee Reginald Mengi mungu amubariki na mzidishie, anapotoa, amekuwa mstari wa mbele sana, kupiga kelele za usafi kutunza mazingira,cha kushanganza wakazi wengi wa dar, ni wachafu, maana sisi wote tuna macho tunamasikio, tunasafiri tunaona, nchi za wenzetu,mazingira yao yalivyo masafi, na ya kimpangilio.

Pia suala la rushwa watu wanaomba tenda, za kutengeneza bustani, za jiji, na kuokota taka, hawapewi mpaka uwe unajuana mtu wa manispaa. au unatoa rushwa, shame shame, kwa uongozi wa jiji, ni wangapi wenye ndugu serikalini,??

Tufike pahala tubadilike, na utuache, ubinafsi, mi binafsi kama mtanzania inanisikitisha kuona Dar kuaanzia AIR PORT,ni uchafu, uchafu , bathrooms toileta aziflash, buibui, wamejaa kila kona vumbi, mvua zikinyesha mapaa yanavuja jengo linatakiwa kipigwa rangi, nothing had been done at all, ni viongozi wangapi wa serikali wanapita kila leo air port,? back & fouth? hawaoni??uongozi wa Dar air port unafanya nini? inahudhunisha, sana, kama mtanzania nina uchungu sana, yanayofanyika, wizara husika, mpoo. pesa zipo za matengenezo zinafanyiwa nini?? air port tv zimeibiwa nobody care, at all sipingi watu kujenga majumba ila jamani ufisadi, umezidi.

Wapo watanzania nje ya nchi na wanatamani kurudi na kuwa na kazi ktk mawizara, ila hawatapewa kazi nikuzungushwa tu, Tuachane nahizi tabia, za ubinafsi tuone mwanga ambao baadhi ya nchi za africa zimeisha uona,

Mazingira ni lazima yatunzwe, na kila mmoja wetu, kuanzia shule za msingi majumbani, mitaani tunapoishi, pia tenda zitolewe na kwa watu wenye uwezo wa kazi siyo ubabaishaji tu jiji la dar, hakuna gabbage dumstar, za kutosha, mazingira lazima yatunzwe, na kulindwa na sisi wote twajuwa fika, kuna vijana, watu binafsi wanatamani sana, kufanya hizi kazi ila hawatapewa, kwa mfano jiji la dar, lina public bathrooms ngapi? na baadhi, ni chafu ukienda ni kuzoa magonjwa, hakuna mabwana afya dar??? wanafany nini?

Upande wa mashule hasa hile za msingi ni marundo ya uchafu yamejaa hapo mbele ya shule hawa wanafunzi tunajifunza/tunawafundisha nini?? hao ndio viongozi wa kesho, wazazi, wakesho tusipowapa mwelekeo wa kuyatunza na kuyalinda mazingira watakuwa raia wa aina gani,? tafadhalini walimu jengeni, mazingira ya usafi mashuleni, kupanda miti, bustani uchomaji wataka, waelimisheni wanafunzi wangazi zote.

Inanisikitisha sana, mi binafsi nilisoma shule ya msingi kijijini, mkoa wa Kagera nilihamasishwa na walimu, na wazazi wangu kuyatunza mazingira, tulikuwa hatutupi taka ovyo, , kuna shule ya msingi karibu na kwa Mtogole maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ina marundo ya uchafu, mitaro imeziba watotto wetu wanavuta hewa chafu yenye magonjwa, hakuna anayeona hilo tunasubiri tume ziundwe, kila mtu ana macho hili suala,.

Pia tunatakiwa kuelimisha, kuanzia mama ntilie, wauza maandazi, wauza utumbo, wauza bucha za nyama, machinjioni,etc unakuta mainzi kibao na mteja bado ana nunua ni uchafu mabwana afya mko wapi mnafanya nini? haya yote ni mazingira ,

Baadhi ya migahawa ina vyoo vichafu vichafu kipindupindu kitaisha vipi.

Zitungwe sheria za usafi ukitupa taka unazoa na fine juu.

Watu wa afya wafanye kazi zao, kuanza na small restaurants za kariakoo, mabaar yana vyoo vichafu, hakuna mfano, maambikizi ya magonjwa yanaanzia huko wahusika mpoo au mpaka tusikie kuna mkubwa nakuja ndio tunafanya usafi, mi mkerketwa wa mzingira na mtanzania ninaye ipenda nchi yangu kwa dhati.
Mungu wabariki watanzania wenzangu, wote na wapenda mazingira.

Ni mimi Mrs.Jossanne George ama Koku.

No comments:

Post a Comment