Thursday, December 12, 2013

PANTONE NAMES RADIANT ORCHID 2014 COLOUR OF THE YEAR



Pantone, a global authority on colour, recently picked Radiant Orchid, a purple hue with pink and fuchsia undertones, as the 2014 colour of the year, replacing the 2013 colour, emerald.

In the upcoming year, the purply rose is expected to influence the world of fashion and interior design.


Each year a colour is selected by a secret committee that draws on global influences ranging from popular travel destinations to technology.


Leatrice Eiseman, executive director of the Pantone Color Institute, says next year's colour is an invitation to innovation. Radiant Orchid “encourages expanded creativity and originality, which is increasingly valued in today's society,” she says.

So how can we inject this pinky-purple radiance into our own homes, without our interior looking too much like a child's bedroom? We took some notes from Australia's top colour experts.

Rikki Stubbs is one of Australia's leading colour designers. Stubbs' career in colour and interior design can be traced back to the 1980s. And today, she runs her own colour consultancy, Pure Colour. For Stubbs, colour is the starting point in interior design. 

Friday, December 6, 2013

RANGI KUBANDUKA UKUTANI.....KATIKA NYUMBA ZETU AMA OFISI ZETU...

Mtakubalia nami kua haya ni matatizo tuliyonayo nyumbani kwetu kwa upande wa rangi kubanduka....katika nyumba hii mteja wangu ameniambia kapaka rangi katika nyumba yake mwaka sasa rangi inabanduka nyumba nzima....kama inavyoonekana hapa...yaani ukishika inabaduka kama unachana karatasi.....

SMOOTHOVER SKIMMING PLASTER......KIBAHA SITE

 Homez deco tukipokea mzingo wa SMOOTHOVER ukishushwa ofisini na kuhakikiwa na kutayarishwa tayari kwa kwenda site ya kibaha......
 tumeagiza ndoo za lita 20 na ziko 22...kwa aakjili ya skimming ndani na nje.....product hi haiharibiki kwa mvua ama jua baada ya kupaka ukutani na haina vumbi jingi kama products zingine na husaidia pia afya ya fundi pia kutopata vumbi jingi....


Wednesday, December 4, 2013

COFFEE TABLE AND CONSOLE TABLE.... MADE BY HOMEZ DECO....

 Homez deco.. kama tulivyowajulisha wadau wetu n wateja wetu kua tunatengeneza fanichure za mbao....hii ni mojawapo ya kazi yetu...hiyo hapo tuu ni coffee table na tumetumia mbao ya mninga na tuka spray rangi nyeusi kama alivyopenda....
hii ya pili ni console table nayo ni mninga meza hii inatumika kama urembo na pia unaweza kuweka funguo ama vitu vidogo vidogo ila unatanguliza kisahani kwanza ndio uweke.....maua pia yanakaa vizuri etc......

Hii unaweza iweka karibu na mlango wa kuingilia ndani ama korido...lakini pia inategemea na nyumba yako ikoje na space pia..


Tunawakaribisha wote...kutoa oda...homez deco

Monday, December 2, 2013

DULUX PRODUCTS........

 Products za dulux kwa ajili ya nyumba yako, ofisi yako etc........Kampuni ya Dulux imeweza kukidhi mahitaji yako ya kuanzia mwanzo wa finnishing mpaka mwisho......ndani na nje........
 Kwa muonekano mzuri wa nyumba yako......tunakukaribisha kupata rangi za Dulux....kwani hudumu na huihimili hali ya hewa yoyote ile....na uzuri ni kua haziwezi kuchakachuliwa kwa njia yoyote ile.......

 Hammerite kwa ajili ya mageti yetu, grills etc......
Hapo juu ndio color chart ya Dulux....hivyo basi karibu tuchague rangi kulingana na upendavyo na utapewa ushauri bure,,,,
 Muonekano wa rangi za ndani na nje....kwa ujazo wa lita 5 na lita 20......lita moja ya rangi ya dulux inapaka sqm..10 kwa mpako wa kwa kwanza...na hufunga mapema..hivyo utahitajika kupaka mara mbili tuu....na huvutuia na muonekano mzuri.....

FOR SALE........


Tunapenda kuwakaribisha wate kua kama una furnitures mbali mbali za majumbani, maofisini.....karibu utangaze nasi...na tutakusaidia kuviuza kupitia blog yetu.....

Huu ni mwisho wa mwaka na natumaini kua wengi wetu, vitu vyetu tunataka kubadilisha majumbani mwetu ama ofisini kwetu.....sasa kwa kutangaza nasi utaviuza na vitasaidia pia kwa watakaonunua.....


Tunatanga mali ambazo hazijaharibika na ziwe katika hali nzuri na ya kuridhisha.......

Katika kipengele hiki nashukuru kua kimeendelea kutusaidia na kuwasaidia wengi wetu....na tumepata vitu vizuri na tunaendelea kuvitumia......


Wasiliana nasi kwa namba 0713 - 920565...

karibuni.....

FURNITURE ZA MBAO.....MNINGA.....ZINAPATIKANA HOMEZ DECO BY ORDER

 Tunawakaribisha wadau, wateja etc. Hapa homez deco kua tumeanza kutengeneza furniture za mbao...aina yoyote ile kulingana budget yako.....
 Tuna design nyingi za kuanzia makabati ya vyumbani, jikoni, vitanda, meza za chakula etc....
 hizi ni baadhi ya kazi zetu....ambazo zimetoka last week kwenda kwa wateja...na vyote hivi tumetumia mbao aina ya mninga....na tumepaka rangi tofauti....dark oak na mahogany.....
 wasiliana nasi kwa kutoa oda na utengenezewe.....




Wednesday, November 20, 2013

FORONYA ZINAPATIKANA HOMEZ DECO........MATERIALS KUTOKA UK NA UTURUKI.....KARIBUNI......


 Size ya foronya hizi ni 45 by 45 na mito pia inapatikana. Mito hubadilisha muonekano wa makochi yako na hupendezesha......
 bei ya kila foronya ni 12, 000.










Monday, November 18, 2013

KAZI YA KUWEKA TILES NYUMBA IKO KIBAHA......

 Homez deco umepata kazi katika nyumba hii iliyoko kibaha ya finnishing ya nyumba nzima mpaka ikamilike.
 Tuliaanza kwa kufanya window shopping na mteja ya tiles katika maduka na tukaipata hii design ambapo wote tulikubaliana tuiweke hii aina ya tiles kwa ushauri wangu.
 Ukiangalia kwa mbali hatujaweka scarting maana tutaweka ya mbao nyunba nzima.

Saturday, November 16, 2013

SOFA SET INAUZWA...............INA MWEZI MMOJA TUU TOKEA INUNULIWE.....NI MPYA KABISAAAAAAA


 Sofa hii inauzwa kwa bei ya 2,900,000/-    ilinunuliwa Orca Deco, sasa anaeuza kwa bahati nzuri anahamishwa kikazi nje ya nchi........sofa iko katika hali nzuri kama inavyoonekana...na tokea ainunue amekaa nayo mwezi mmoja tuuuu.Color ni Dark brown, purple na cream....

Wednesday, November 13, 2013

FINNISHING YA NYUMBA ZETU........



Wengi wetu tumekua tukidhani kua kazi nzito ni ujenzi wa nyumba na sio finnishing,,,,naomba kuwaeleza leo kua sio kweli kwa asilimia flani........

Jamani finnishing ya nyumba ni gharama kuliko ujenzi....tutambue hilo, na utakuta wengine mpaka miaka kadhaa hawajamaliza, kwa kua wanajua nini wanafanya ...

Kinachohitajika ni kujipanga, na kutafuta mtaalam aweze kukusaidia katika hili....unaweza kujenga nyumba yako vizuri...lakini ukija kwenye finnishing unaanza kubania hela na kutaka virahisi...yaani jua kua nyumba unaiharibu na hutokua umefanya kazi yoyote ile......nyumba itakua mbaya mbaya na unaweza kujuta.....


Tujitahidi katika hili kua kama najenga nyumba yangu basi ni afadhali nifanye taratibu kwa ufasaha kuliko haaraka haraka na ukaharibu kazi......

Tujitahidi kua wavumilivu katika kumaliza nyumba zetu kuliko haraka haraka, ninasema hivyo kwa kua nakutana na watu kama hawa, na kwa kweli katika kazi yangu sipendi haraka ya kupitiliza kabisaaaaa.......

Kazi ya designing inahitaji muda na nafasi. bila hivyo ni kuharibu kazi.....nami sipendi hilo litokeeee....

Kwa kwetu Tanzania bado tuko nyuma katika hili ingawa tunajikongoja na tutafika kwa kuelimishana na kuelewana...

GRILLS DESIGN......

 Tunayo furaha kuwatangazia kua tumeanza kutengeneza grills za madirisha na milango.  Hizi ni baadhi ya designs tulizonazo, na tutaendelea kuwaletea designs nyingi kadri tuwezavyo......

TUNAOMBA JIBU LA SWALI LAKE KWA MDAU MWENZETU........

Naomba mnisaidie jinsi ya kuosha madumu( vyombo) vya kuhifazia maji, nimetumia njia mbali mbali but naona bado ile rangi ya kijani imekataa kutoka, yanaoneka machafu kweli coz ni meupe na mkono haupenyi ndani..
thanx, mdau wa Arusha.



Monday, November 11, 2013

KWA WALE WOTE WENYE WATOTO WATUNDU WANAOCHORA MAKOCHI........RANGI ZINAZOFAA ZA MAKOCHI.....

 Habari za muda kidogo wadau wangu, nilikua kimya kutokana na majukumu ya kifamilia kidogo, na sasa tuko sawa.

Sawa, sasa kuna tatizo kidogo, kwenye uchaguzi wa makochi ya kwenye nyumba zetu, kwa wenye familia ya watoto wadogo, kwanza kabisa ninachoweza kusema ni kua mtoto ukimfundisha anaelewa, na ukimdekeza atakupa hasara..........sasa ni wewe tuu uamuzi wako.......

Nimekutana na tatizo hili la makochi kuchorwa chorwa na watoto wetu, na jamani bei za makochi tunazijua zilivyo gharama........na pia kwa kua tuna watoto basi hatuna budi kununua makochi ambayo rangi zake ni dark na sio light.......kupunguza tatizo la watoto wetu kuchora kwenye makochi yetu.....

Hebu fikiria umenunua kochi lako kama ndio off white ama cream then likachorwa chorwa na mtoto, kama ni cartoons ama ndio anajifunzia homework etc......

JIBU KWA MDAU







Naomba kumjibu mdau wangu aliyekua ananiuliza kua hii meza ipo.na jibu ni kua meza ipo, na imebaki moja tuuu.....bei ni 1,250,000/=

Karibu tuwasiliane, na samahani kwa kuchelewa kukujibu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu.





Monday, November 4, 2013

Thursday, October 10, 2013

KABATI ZA JIKONI KATIKA MUONEKANO WA 3D

Katika muendelezo wa ku design 3d upande wa jikoni.



Naomba niwafahamishe wadau wote kua, kabla ya kufanya design ni lazima tujue kua jiko hili litatumikaje? na eneo letu litatutosha?  kuna aina mbili hapa, kuna jiko ambalo tayari limesha jengwa, na kuna lingine ambalo bado halijajengwa.

Kwa hili ambalo limejengwa tunachokifanya ni kucheza na space iliyoko katika ku design........

Ambalo halijajengwa tutaanza maandalizi, na kidogo hii hua nirahisi zaidi, ambapo tunahitajika kujua ni watu wangapi watahitajika kuwepo katika jiko letu, na je watapishana vizuri, na je nafasi itahitajika kiasi gani kwa ajili ya makabati, jiko, sink, fridge etc....

Nakumbuka kipindi cha nyuma nilishawahi kuzungumzia aina za majiko, na utachagua jiko lako liweje kulingana na ukubwa wa eneo lako la kiwanja. na hata kama limesha jengwa basi itaaangaliwa ni design gani inaweza kufaa kwa jiko lako, na kama kutakua na marekebisho madogo madogo basi yatafanyika ili kuweza kuwekwa sawa.

Wednesday, October 9, 2013

MORE 3D DESIGN,

Tunaendelea ku design kwa 3d kwa wateja wetu........na hii husaidia kujua fanicha zikaeje, rangi ziweje, floor pia iweje,  mapazia ya rangi gani etc......

DAY BED....AVAILABLE BY ORDER @ HOMEZ DECO....(hardwood mkongo & mninga)

 Day bed hutumika kwa kupumzikia, unaweza kukiweka sitting room, balcony, ama kwenye korido kama ina nafasi......

Thursday, October 3, 2013

3D DESIGNS......



3d ni michoro ambayo huchorwa kwa kutumia computer na software maalum, ili kuweza kuona ni jinsi gani jengo lako itakua tayari baada ya kujengwa, na muonekano wake kwa ujumla, mpangilio wa fanicha ndani, na kuweza kukuonyesha makosa madogo na makubwa......

Hapa chini ni baadhi ya michoro ya 3d, ambapo tumeweza kuonyesha mfano wa nyumba itakavyoonekana baada ya kwisha kujengwa kwa nje....

3d yaweza kua niya garden, ya nyumba nje, ya mpangilio ndani, etc....ni wewe mwenyewe unahitaji nini.....


 Katika kazi yangu hii nimekua nikikutana na makosa mbali mbali ambayo wateja wangu wamekua wakiyalalamikia, kwamba jiko limekua ni dogo, ama chumba kidogo. ama hakutaka muelekeo huo.....mara vipimo havieleweki, rangi sio nzuri.......mpangilio wa fanicha. vitu haviendani. switch za umeme hazikuaa sehemu husika...etc.....ni tatizo kwa kweli......

Kitu kingine nimegundua kua katika ujenzi wa nyumba zetu, hua hatuna ule utaratibu wa kua wawazi kwa archtects(wachora ramani). Hausemi nini unataka, yaani we umeona nyumba ya flan basi unataka kua kama na yake na inabadilishwa kidogo tuuuu.......(copy and paste).

Jamni designs za nyumba ziko nyingi mno.....na ndio maana utakuta hapa kwetu nyumba zinafanana mno.......ukiona nyumba imebadilika basi ujue hiyo nyumba mwenye hakai sana hapa, kaja na mchoro wake toka nje.....

(nitalizungumzia hili siku ingine kwenye mada yake) inafika kipindi tuambizane ukweli....sasa......(let's be creative)

 kwa upande wa 3d, kama tungekua tunafuatilia ama kujua mapema, wengi wetu tusingekumbana na matatizo haya....maana saa ingine utakuta ukuta umezidi, inabidi kubomoa.......sasa hizo ni gharama zisizokua na maana.......

Tuesday, October 1, 2013

MAANDALIZI YA MWISHO WA MWAKA KATIKA NYUMBA ZETU.......

Wengi wetu tumekua na kawaida ya kujiandaa kwa ajili ya mwisho wa mwaka, kama kwenye maofisi basi tunapamba ofisi zetu kwa mapambo, na kama ni kwenye nyumba zetu basi nako tunajiandaa kufanya maandalizi.

Asilimia kubwa kati yetu ni kua hua katika kipindi hiki hua tunajitahidi kumalizia nyumba tunazojenga ili tunahamia, na wengine tunahamia kwenye nyumba zengine za kupanga....kubadilisha mazingira....etc.

Katika yote haya maandalizi yanahitajika.......na inategemea pia na nyumba yenyewe inahitaji nini.....

Kwenye upande wa matengenezo, ama rangi, etc....

Bila kusahau pia fanicha, nazo pia inatubidi tuangalie, kama zinahitaji marekebisho, ama zinahitaji kubadilishwa kabisaaa.....yote haya yanaanzia kwako na wewe mwenyewe.

Katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ndio wengi wetu tanaangalia je yale malengo yetu tuliyoyapanga kwa mwaka mzima yamefanikiwa, ama yalikaribia kufanikiwa.

Napenda kukumbushia kua hiki ndio kipindi cha kufanya maandalizi ya nyumba zetu......kwa usafi, kutoa vitu ambavyo hauvihitaji na kugawa, na kama kuna vitu vibovu basi ndio wakati wake wa kuviteketeza.....

Pale ambapo unapopanga mikakati yako ya kimaendeleo, tusisahau na nyumba zetu.....

Jamani nyumba nazo zinahitaji service.....yaweza kua ni ya kila mwaka, ama ya baada ya miaka kadhaaa....ni wewe mwenyewe ndio utaangalia nyumba yako iko katika hali gani.....

Tumekua tukijisahau sana kwa upande wa kufanyia service nyumba zetu.......na mwisho wa siku unakuja kukuta matengenezo yanakua ni gharama zaidi ya matarajio yako..........wakati ungekua unafanya service ungeepuka tatizo hili la gharama mara dufu......



Tuesday, September 24, 2013

MALI MPYA ..........ZINAPATIKANA HAPA HOMEZ DECO.......WASILIANA NASI KWA MANUNUZI - 0713 - 920565

Tunapenda kuwaarifu wadau wetu, wateja wetu na wote kua sasa Homez Deco tuna mali mpya ya sofas na meza za Tv za kisasa........

 Sofas zote bei ni 3,400,000/-  ( bila kusahau discount ipo....)
 Hizi ni sofas zote tulizo nazo.......kulingana na mahitaji yako na space uliyonayo........

Thursday, September 19, 2013

PROJECT IFUATAYO............


HALIMA KIGUA SIKU YA KITCHEN PARTY YAKE.......

 Hii ilikua ni siku ya Halima Kigua.....kitchen party yake........hapa akiwa na baadhi ya marafiki.....kulia ni Jennifer na kushoto ni Faith......akiwa anaingia ukumbini....