Friday, December 11, 2009

Huwa ninatimiza ahadi nilizoombwa!!

Niliombwa na mdau wangu mmoja kuwa anaomba nimletee designs za garden house, ama sehemu ya mapumziko kwenye upande wa garden ila iwe ni ya makuti.
Sasa basi nimemtimizia maombi yake, ila sasa nimeleta designs nyingi ili wengi wetu tuweze kuwa na aidia zinafananaje. Natumai nimejibu ombi lako.



























8 comments:

  1. Hai mad sylvia,

    Habari za siku kidogo, natumaini unaendelea vizuri na shughuli zako za kila sk.


    Nimependa style za bustani na napenda saana nami nipendezeshe kwangu ila kinanikwamisha kitu kimoja, kwangu sina fance pia sijajua kama naweze kutengeneza bustani endapo hakuna fance.

    Isitoshe tuko barabarani magari yapita sana hivyo kila apitae anaona hapo kwangu, hata ukiwa unafanyaje lazima akuone.

    Naomba unisaidie kama inawezekana na je ni kwa style ipi utafaa zaidi.

    Mwisho naomba ufungue blog ya lady jay dee kwenye picha za party akiwa na rafiki na wadau
    utaona kuna meza iliyo na vinywaji alafu kuna kaka amesimama nyuma ya meza yaani nimeipenda saana pengine unaweza ukawa nazo au unisaidie wapi naweza kuipata.

    Kikubwa zaidi ni upande wa garden.

    Ahsante
    mama brian
    mwanza

    ReplyDelete
  2. mama B, mambo!!! jamani umekuwa kimya muda kidogo. karibu sana, mu wazima mwanza? sie huku tu wazima ila ndio mvua mvua tuuu kiasi.

    Kuhusu meza unayoiongelea ni hiyo ya counter ambayo amesimama kaka anamimina vinywaji, sio, hiyo sitaweza kuitengeneza ila nitakutafutia halafu nitakujulisha bei yake na wapi yapatikana.

    Kwa upande wa garden hilo halina shaka ila ninaomba uipige picha nyumba kwa nje ndio niweze kukusaidia, kama ungekuwa dar ningekuja kwako. ila uko mbali, ninataka kujua kunaumbali gani kutoka kwako mpaka barabarani, je kuna mtaro, na kama uko umeacha nafasi gani, yaani kuna maswali ambayo yanahitaji kuona nyumba yako halafu ndio niweze kujua ni namna gani ya kukusaidia na ni maua gani.Ingawa umeniwahi kwani j3 ninataka kuongelea kuhusu garden.

    Asante sana mama B.

    Weekend Njema.

    ReplyDelete
  3. Huku wote wazima kabisa, pia mvua zinanyesha ila sio sana.

    Kuhusu mtaro hakuna vile vile nitapiga picha nikutumie hata iwe rahisi kwako kunisaidia.

    kwani we hutaki kuja mwanza jamani??? au we si wa huku? tafuta siku uje utembelee rock city.

    kwa upande wa meza sawa nitasubiria jibu toka kwako. ngoja nitafute mpiga picha akanipige kisha niitume.

    Bye Bye
    mama brian.

    ReplyDelete
  4. Mama B utakuwa umenisaidia kwa kunitumia picha. huko rock city ni kwetu wotee nitakuja tuuu nikipata likizo si unajua mambo ya kazi na biashara? lazima ni balance.

    ReplyDelete
  5. Unajua nilitaka kukuuliza kuhusu mrs. Jossane George mlikuwa mmepangaje kuhusu kutusaidia mambo hasa kwa upande

    bustani? je mtufundisha through humu au mtatembelea baadhi ya sehemu zilizo karibu?

    Nimependa wanavyofanya kazi na mr. wake kwa ushirikiano na upendo.

    mama brian

    ReplyDelete
  6. kweli kabisa inabidi uvizie mda wa likizo ndo upange uje au vp madamee?

    sasa nipige kwa mbele au na ubavuni? maana kuna nafasi tutaiacha kwa ajili ya kutengeneza kitu kama duka kwa baadaye pia utatusaidia mawazo maana hilo duka litakuwa baada ya miaka ijayo pakishacha

    ngamka.

    mama brian.

    m

    ReplyDelete
  7. naomba upige picha eneo lote la kuzunguka nyumba na uniambie ni eneo gani ambalo mmelichagua kwa ajili ya kujenga hizo frem ili hata tukipanda maua basi yasiwe ni ya gharama na muda mrefu na wakati mkiwa tayari kujenga basi shepu ya garden isiharibike.

    Kuhusu Mrs. Jossanne George bado tuko kwenye mchakato, maana kama atahitajika kwa mikoani inabidi tuangalie na gharama zake pia, si unajua tena uchumi uko juuuu.

    Ila nitakuwa nina ku update mamaa yangu.

    ReplyDelete
  8. thawa kabitha,

    mama Brian

    ReplyDelete