Monday, December 14, 2009

NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZANGU, KWAKO DADA SYLVIA

Umekuwa mchango mkubwa, sana, ktk jamii yetu, kutuelimisha, masuala mbalimbali,ya kimaisha, kimazingira,najuwa kuna baadhi ya wakina mama, wakina dada hata wakina, baba, wamepata mwanga wa kujua masuala ya upambaji, wa ndani ya nyumba zetu, na nje, mi kama mchangiaji mwanajamii, natoa shukurani zangu za dhati.

Ni kweli kuna baadhi ya watu, binafsi, mashirika,familia, na wengine wengi tu, wana majumba majumba mazuri, sehemu za biashara ila, interior designing ya ndani ya nyumba ni, kizaazaa, maana kuna watu rangi zinawatatiza, sana. na mpangilio mzima, kwa upande wa sisi watu tuilo wengi uwa atutilii maanani, sana,mpangilio wa rangi, mapambo, furnitures, enterteining ,centers, picha za ukutani, tuna makolokolo kibao.

Utakuta sitting rooms nyingi zimejaa, madoli, tedy bears, hii ni big don't, kwa wote, wale wenye vitu kama hivi , una madoli michezo ya watoto siyo siiting room, kuwa na sehemu maalum, kama vikapu, ifadhi vitu vyote kwenye makapu,

Tujifunze kuwa na vitu vichache vyenye mpangilio mzuri,unaweza kuwa na nyumba ndogo tu ila yenye mpangilio mzuri tu na ya kuvutia, pia wapendwa kuweni na tabia ya kufungua madirisha, hewa safi ni muhimu sana, ndani ya nyumba zetu, vyumbani, bafuni, sebuleni, hakikisha unapata hewa safi, siyo tena, inakuwa giza.

Punguzeni mrundikano wa vitu,visivyokuwa na ulazima, kwa mfano wapendwa, hakuna haja ya kuweka makochi machakavu, vitanda vibovu, nguo marundo, utadhani wakimbizi, tuwe na utaratibu mzuri silazima uwe na makabati ya gharama kuweka nguo kuna makapu makubwa hifadhi nguo zako, unakuta baadhi wanahifadhi nguo kwenye mabox, hiyo ni big don't, kwani ndio mwanzo wakukaribisha panya ndani ya nyumba, na nyoka, etc.

Mara nyingi tuna kasumba moja kuwa nyumba yenyewe ya kupanga, siwezi kipendezesha ila elewa wewe ndiye unayeishi hapo usiposafisha choo, bafu, jiko, magonjwa hayataenda kwa land lord wako ni wewe utakayenda hosptali.

Regards,
Mrs. Jossyane George.

Hayo ni machache kutoka kwake, amenitumia emal jana jumapili nikaona si vibaya nikaileta kwenu walengwa, na namshukuru sana kwa support kubwa anayonipa. Naona leo kaamua kunisaidia kwenye interior designing, thanks a lot sis.

1 comment:

  1. Asante sana dada Silvia..na mdau alietuma email...ametusaidia kwani wengi wetu hatujui mpangilio wa nyumba zetu...
    hiyo ni tips nzuri kama nyongeza...
    Ila mie ningependa kujua aina ya rangi ya makochi na rangi za kuta katika kuchanganya ili nyumba iwe nzuri nadhani ungetusaidia kuoanisha rangi hizi dada silvia..
    Asante Dorothy

    ReplyDelete