Monday, December 7, 2009

Jiji La Moshi

Nimepata simu kutoka kwa mdau mmoja yeye yuko Jiji la Moshi anasema kuwa sasa hivi Moshi imekuwa kama vile nchi za wenzetu zilizoendelea kwa usafi,

Siku hizi ukitupa karatasi hata la pipi ama ukitema mate ni unakamatwa na unalipishwa faini hapo hapo na askari wa jiji na wengi wao wanavaa nguo za raia hivyo huwajui. Sasa wao waweze wananini na sisi tushindwe tuna nini jamani? Wote si tuko Tanzania hiii jamani?

Jamani Dar inawezekana kuwa safi na kuwa na mazingira mazuri na miti yenye kivuli ama green city wenzetu wanavyoita ila ni mimi na wewe kuamua.

Sasa basi nawaomba tuendeeleee kushauriana na kupeana mawazo halafu ndio tuende kwenye ngazi husika tukiwa tuko tayari kwa mapambano dhidi ya uchafu na kuweka mazingira yetu vizuri na salama kwa afya zetu.

2 comments:

 1. My compliment for your blog and pictures included,I encourage you to photoblog

  CLICK PHOTOSPHERA

  Even week another photo album

  Greetings from Italy,

  Marlow

  ReplyDelete