Friday, February 17, 2012

HUU NI MWANZO WA UANDAAJI WA BUSTANI AMBAZO TUMEZIFANYIA KAZI, FROM JOSSYANNE - USA

STEP 1: UTAYARISHAJI NAUPANDAJI WA MAUA BUSHES, AND SHRUBS, HATUA YA KWANZA
Kuondoa magugu majani ambayo yahatakiwi   ktk bustani kama mnavyoona hapo, ni kama shamba  tu unalimia unaondoa,visiki magugu  na majani ambayo hayatakiwi, so iwe ni kwenye shamba au bustanini. 
 

step 2: ikiishaondoa magugu na kusafisha, bustani,

kwa huku usa uwaga tunatumia plastic garden tarp, hii  ni envromnental friendly, ina fyonza maji, inavifadhi unyevu unyevu, so inasadia mimea kukua vizuri kama mvua zikinyesha inahifadhi maji, kwa muda mrefu,
  pia siyo kama mifuko ya rambo ambayo hat aukifukia bado utakuwepo ardhini kwa muda mrefu  hii ni maalum, kwa gardens za aina zote ziwe za mboga mboga matunda au maua miti au vichaka vifupi, na cha msingi zaidi hizi plastic tarp zinazuia magugu ambayo mara nyingi yanauwa mimea au maua, kama mnavyoona hapa hiyo ndio plastic tarp kwa hapo Tanzania uwaga hatutumii hizo tarps, pia hatuna hizo
  plastic garden tarp kama zitakuwepo ni wachache wanaojua kuzitumia. 
 

 
 
 

STEP 3: Bado tuko kwenye uandaji wa bustani, za aina mbalimbali

Ni vizuri, landscapers wenzangu kuwa na vifaa, tunaita landscapers gears, inakurahisishia kazi na muda,
  wengi wenu hamna vifaa basi kazi inachua muda mrefu, kumalizika, step ya tatu ni kuweka mbolea hapa
 Usa, kuna mbolea za aina nyingi tu kuna za wanyama pia kuna hizi ambazo zinatengenezwa, kutoka na miti majani mpaka mabaki ya wanyama ninaposema wanyama ni kwamba, roads kills wanyama wanaogongwa barabarani hasa deers yaani swala uwaga wanachukua wanawachanga na miti majani wanatengeneza mbolea inaitwa mulch, wenzetu, wamepiga sana hatua ktk suala la mazingira, na pia wanayapa kipaumbele siyo sisi kuvaa, Magari ya kifahari  ila ukiangalia majumbani tunapoishi na mazingira yanatuzunguka, ni hatari tupu
wadau tuyapende mazingira yetu kwa ujumla, na kuyalinda . Kama mnavoona hapo kwenye picha ukiwa na vifaa ni inakurahisishia kazi ni mimi hapo nikiweka hiyo mbolea aina ya mulch kwenye bustani ambayo tuliianda na hiyo mulch ni kama wengi wenu mnavyochanga mbolea na udongo na sisi huku uwa tunaweka mulch juu ya hiyo tarp plastic then una fanya laking unasawadhisha  mpaka iwe leved.
  

 nadhani wadau ambao mnapenda kujifunza, na kuelimika jifunzeni tutaendelea, tena asante. 
 

 

 
 

1 comment:

  1. Hallow there mm ni mpenzi wa blog hii hongereni kwa kazi nzuri ninapenda kuifuatilia hii article ya mazingira ningefurahi kama ingeendelea ili nijifuze zaidi asante Mungu awabariki sana

    ReplyDelete