Tuesday, October 12, 2010

Strechmark za kwenye tumbo wakati wa ujauzito

Napenda ku share na wadau wangu habari njema, ni kwa wale wote ambao ni mother to be na ambao watakao teegemea kupata watoto.

Hizi streachmarks kwenye tumbo, nilikua ninazisikia tuuu, ila nakumbuka siku moja wakati niko kwenye first trimester, nilikwenda mlimani city kwenye maduka ya watoto nikiwa ninafanya window shopping.

Nikaingia duka la mummys, nikafanya window shopping yangu, na wadada wa duka hilo ni wakarimu na walinihudumia vizuri, kuna dada mmoja muhudumu wa duka hilo akaniambia dada naomba nikupe ushauri kuhusu kukabiliana na strechmark, ndio akaniambia kua mafuta ya mgando, yaani vaseline, baby care etc hua yanasaidia sana.

Cha kufanya, paka tumboni mafuta hayo mengi ya kutosha tokea mimba ikiwa changa kila siku mara baada ya kuoga. Inasaidia sana kupunguza kuwasha na kutotoa strechmark

Akanionyesha tumbo lake kweli halikua na strechmark yoyote, na mtoto wake that time alikua na miezi 4.

Kweeli nilichua ushauri wake na kuufanyia kazi mara moja. YAANI HAMUWEZI KUAMINI ILA NDIO HIVYO SINA STRECHMARK MPAKA SASA NA  NIKO SECOND TRIMESTER, NA KUWASHWA TUMBO NI MARA CHACHE. NINAMSHUKURU SASA YULE DADA KWA KUNISAIDIA (KWA KWELI KAMA NINGEWEZA KUWAONYESHA TUMBO LANGU NINGEWAONYESHA MJIONEE ILA UTAMADUNI HAURUHUSU KWA KWELI)


8 comments:

 1. Habari mama kijacho,

  Mimi ni mama wa mtoto mmoja, nilitaka kutoa ushauri kuhusu hiyo michirizi.

  Sababu kubwa ya kutokewa na michirizi inategemea na what kind of food unachokula kabla, na wakati wa ujauzito. Mimi sikupaka kitu chochote na sijatokewa na michirizi yoyote, bse wakati nina mimba nilijitahidi kula vitu natural sana mfano ugali nilikuwa natumia unga ambao haujakobolewa, matunda, mboga za majani ambazo nimezilima mwenyewe, na nilihakikisha chakula chochote nilichokuwa nakula kimeandaliwa nyumbani na sio cha kununua, kama ni mayai ya kienyeji, nilikua nafanya mazoezi yakutembea sana, nilkua nakunywa sana juice ya viazi vijulikanavyo kama bitroots kwa ajili ya kuongeza damu mpaka wakati karibu najifungua damu yangu ilikua 13 na wala sikupata kizunguzungu mara baada ya kujifungua, hivyo mbali na kupaka hayo mafuta pi ajaribu kula vitu natural

  ReplyDelete
 2. Namshukuru Mungu naendelea vizuri, asante kwa ushauri wako, mi jamani ugali imetokea kwa kweli siupendi ila nakula hivyo hivyo mara chache chache.

  Kwa kweli hua ninafanya mazoezi ya kutembea mara kwa mara, na pia ninakunywa juice ya rozela natengeneza mwenyewe, na kuna dawa niliyopewa clinic ya kuongeza damu inaitwa HB Tone, na mboga za majani. matunda bila kusahau.

  Kwa ujumla ukishakua mama mjazito jitahidi kula vyakula natural.

  Inanisaidia asana namshukuru mungu kwa yote mpaka sasa.

  Tunaendelea kukaribisha maoni yaweze kutusaidia wanawake wote.

  Asante kwa ushauri my dear.

  ReplyDelete
 3. kuhusu michirizi, mimi nilitumia mafuta yanaitwa SAMONA yanatoka UGANDA. Ni ya mgando but si mazito mepesi hayaleti jasho kabisa. Kama unayopaka yanakuletea jasho nunua haya ni mepesi sana.Mi tu mbo langu utafikiri sijazaa. Na sasa ni mother to be of 8 weeks mimba, nimeshayanunua. Kitumbo kikitoka nitakutumia picha.Tuwe tunajulishana maduka mazuri for nguo za kuvaa jamani si unajua sisi mama vitumbo inabidi tupendeze

  ReplyDelete
 4. Hivyo viazi nitavipata wapi, last time nilisumbuka sana na damu, pamoja na rozela juice ya tembele bichi but damu ilikuwa ndg nijulishe sitaki kupata tabu this time

  ReplyDelete
 5. Hi asante kwa kushare nasi anonymous wa pili, na hongera sana my dear. sasa naomba utujulishe ni wapi mafuta hayo yanapatikana ili, nasi tuweze kununua.

  Kuhusu nguo so far mimi binafsi hua ninachanganya za madukani na mitumba, maana nimekulia kwenye mitumba nisiseme uongo. Kuna huyu kaka yuko mwenge ndio hua ninanunua sana kwakwe, anaitwa sammy namba yake ya simu ni 0719 - 925 201, mitumba yake anatoa nairobi 1st class. Nitafanya research zaidi ya kujua ni maduka yapi yana nguo nzuri na kwa gharama nafuuu.

  ReplyDelete
 6. Hi anonymous wa tatu, na pia hongera my dear. mimi hua ninachanganya nguo za madukani na mitumba maana ndio iliyonikuza, mtafute huyu kaka anaitwa sammy yuko mwenge namba yake ni 0719 - 925 201. nguo zake anatoa naoirobi na ni nzuri sana sana.

  HB Tone ambayo mi natumia kwa kuongeza damu na niliandikiwa na doctor wangu, ila endelea na mboga za majani, rozela, zitakusaidia usiziache, nitawauliza wadau watusaidie. pia zinapatikana kwenye maduka ya dawa, kuna ya syrup na ya vidonge, zote ni sawa. Mungu atakusaidia

  ReplyDelete
 7. Hi sylivia hongera sana,when is your baby due?wa kwangu ni end of Jan 2011

  ReplyDelete
 8. wow! me too end of jan 2011. mimba yangu ya kwanza sikua na stretch marks, nilipojifungua tu, after 1 or 2 days nikaziona, so kazana kupaka mafuta hata baada ya kujifungua, unaweza usizione ukiwa mjamzito, ukijifungua tu tumbo linaposinyaa uzione. sikua na paka chochote kipindi hicho, maybe ningetumia mafuta flani flani nisingekua hivi sasa hivi

  ReplyDelete