Wednesday, February 8, 2012

JAYDAN HAS REACH 1 YEAR TODAY 8/2/2012. Happy Birthday my son.....I love you.....Mungu akubariki na kukuepushia mabaya.....
Hi all, napenda kumshukuru mungu kwa kila jambo analonitendea, mimi na jaydan, kwa kweli sintotaka kua muongo, nimepitia katika, mabonde, milima, etc.... Lakini mungu yuko nami mpaka sasa na anaendelea kua nami.


Nawashukuru pia wadau wangu kwa kua nami katika kipindi hiki chote, cha mpaka mtoto wangu Jaydan amefikisha mwaka 1, kwani mmenivumilia, na kuniamini na kunipa kazi zenu, na ninazifanya kwa usahihi mkubwa.

Nakumbuka nilivyokua mjamzito, nilitoa picha yangu, hapa kwenye blog, kuna mdau ali comment kua, sylvia usidhani ni rahisi kua single mum..... baadae nilijiuliza, bila majibu, ila kadri siku zinavyozidi kwenda, nilikuja kuelewa nini alimaanisha,..

Kweli kua single mum, ni kazi, ila nimejifunza mengi, kupitia mtoto wangu, kwani kwanza ninafanya kazi kwa bidii nikijua kua nina mtoto ananitegemea, mtoto wangu ndio faraja yangu hapa duniani, emagine ninarudi nyumbani nimechoka, jayd wangu ananipokea, nina hasira zangu, jay ananichekea, yaani ni raha kweli.....HALAFU KITU KINGINE, JAYDAN WANGU NDIE ATAKAEKUA LOVE TEST WANGU, KWANI AKITOKEA MTU ANANIPENDA, KWANZA NTAMWANGALIA KAMA ATAMPENDA MTOTO WANGU, NA SI UNAJUA KUNA YALE MAPENZI YA KUJIFANYISHA, NTAMBALASA... NA KAMWE SITAMUACHA MTOTO WANGU KWA MTU, KOKOTE NIKO NAE ETI SIO KESHO NAOLEWA NAMUACHA MWANANGU KWA MTU........PATACHIMBIKA....etc..

Leo Jaydan amefikisha mwaka 1, nina furaha isiyo kifani, kwanza kua mama, na pili ninajitahidi ku balance muda wa kazi na mtoto. ninaanza ku save hela ya shule yake,.... jamani ukijipanga hata mungu anakuona na atakusaidia, nakuhakikishia huto oomba hela kwa mtu, unajikuta tuuu maisha yanakwenda smooth...

Sasa basi napenda kuwahusia single mothers wote, kua wasilalamike, wala kunung'unika, kwani mungu ndie mpangaji wa yote. Hebu jiulize ni wanawake wangapi mpka leo wanatafuta watoto, na hawajapata, ila wewe mungu amekubariki na umepata mtoto? Na haujapata mtoto na wote uliokua nao ukapata mtoto na huyo uliezaa nae? Na ujue wewe si mgumba....MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO.....

Mimi niliweka mikakati na ambayo inanisaidia sana mpaka sasa, nimepunguza matumizi yasiyo na maana, nilikubali kujishusha, ninasikiliza ushauri, ninajishughulisha na kazi zangu yaani sina muda wa kufikiria mwenzangu anafanya nini na yuko wapi.......ama kwenda kumfanyia fujo....huo muda sina kabisaaaa,


Nawashukuru wale wote walio kua karibu nami katika kipindi hichi chote, na bado wako nami,,,Halima, Phides,Sylvia,Jossyanne,Nuru the Light, Dina, na familia yangu.

Jua kua wewe ni single mother, unaweza na utaweza, wewe ni mzuri, kubali kua uko peke yako, na mtoto ni wako....... na muombe sana mungu akutangulie katika kila jambo.........it's hard but you can make it without him .....hongereni kwa kua na watoto........ Nawapenda wooteeee

9 comments:

 1. Hongera sana Jayd kwa kutimiza mwaka mmoja, nakutakia maisha marefu yenye furaha. Hongera kwa kuwa na mama anayekupenda sana na kukujali. Mwenyezi Mungu akukuze kiroho na kimwili. Sylv Mungu akusaidie katika malezi ya Jaydan.

  Ritha

  ReplyDelete
 2. Congratulations Sylvia for being a strong and hardworking single mom. I envy you, your work, and strengths. I am a single mom myself, lost my husband some few years back but that was not the end of the world, actually it was the beginning of a new chapter of life. I worked hard, went back to school to acquire more knowledge, sharpen my career and break the glass ceiling. I consider myself happy and successful today because God has granted me more than I ever asked for. It's possible to be yourself and succeed, kinachohitajika ni NIA (Determination), kujituma, na kuamini unachokifanya. I consider myself independent, sihitaji sumni ya mtu especially from a man hahahhah na ukianza kujituma heshima inakuwepo...WOMEN POWER, kina mama hoyeeeeeeee! Anyway, happy birthday to the cute little angel, Jayden! YOU ARE ONE TODAY. MAY GOD GRANT YOU MORE, AND MORE, AND MORE......infiniti!

  ReplyDelete
 3. HONGERA SANA MANENO YANALIZA HAYO MPENZI BUT KAZA BUTI MAMA UNAWEZA PIA UNAWEZA KUWA NA HUYO MUME IKAWA MATESO MAKUBWA SANA NDANI YA NDOA UKATAMANI UNGEKUWA MWENYEWE TU..

  ReplyDelete
 4. such a toung words..hongera Mungu azidi kumlinda mwanao na wewe pia..love ya...ellyka

  ReplyDelete
 5. Hapy birthday Jaydan.
  Ila humtendei haki mtoto kwa kutomjua baba yake.Mtoto abahitaji malezi ya baba na mama hivyo usijifariji kwa kuwa single mama is not easy at all. Mtoto atajisikiaje anaposikia wenzie wanaita baba?

  ReplyDelete
 6. AnonymousFeb 8, 2012 08:45 AM Naomba ufikirie kabla ya kukurupuka na kuongea. Aliyekwambia Jaydan hamjui baba yake ni nani? Unajua not always kwakuwa una mimba ya mtu then umng'ang'anie hata kama mmeshindwana. You do not know kwanini Sylvia hayuko na baby daddy wake. Na wao kutokuwa pamoja does not necessarily mean hayuko kwenye maisha ya mwanae. Pengine wana agreement yao ya when he can see the baby. Nyie ndio wale wale kitu hakiwezekaniki UNALAZIMISHA just because you cannot be alone unaona maisha yana revolve around a man regardless kama relationship ina work au la! Zama za kizamani zishapitwa na wakati, sasa hivi kama imeshindikana you move on because YOU CAN MAKE IT WITH OR WITHOUT HIM!

  ReplyDelete
 7. Anonymous Feb 8, 2012 08:45 AM.Sasa ulitaka afanyaje?amchukue mtoto ampeleke wa baba ama?au amlazimishe baba kumlea mtoto?Fikiria mara mbili kabla ya kuandika au kuongea.Kama wewe mumeo analea mwanao shukuru Mungu pia.Ila naamini hata mtoto akikua ataelewa kwani watoto waliofiwa na wazazi wao hawakui?
  Mumy mpenzi usikate tamaa Mungu tu ndio atakayekukuaia mwanao na si baba wala nani!go on girl

  ReplyDelete
 8. mama Mkubwa Linda.February 9, 2012 at 2:07 PM

  Happy bday champ, i can feel ur mom's words, cant say anything ila Mungu anaona mama yako alivyo strong na anavyohangaika, Sylvia mdogo wangu, Mungu ni mwema, mtoto anakuwa na ataishi vizuri kwa nguvu za mama yake. Anonymous hapo juu, kuwa single mom haimaanishi mtoto hamjui baba, yake, anaweza akawa anamjua lakini hana msaada wowote kwa mtoto, wanaume wetu wanajua zalisha tu, likifika swala la kulea wanajidai wako buzy. Slyvia im proud of u lil sis.

  ReplyDelete
 9. sasa mama Jaydan afanyaje ukisema hamtendei haki mtoto?amlazimishe m2 aishi nae ili mtoto aweze kumuita baba au akachukue ligubegube ili mtoto aweze kupata m2 wa kumuita baba?hebu rudia kusoma alichoandika utaelewa zaidi.mama E

  ReplyDelete