Tuesday, February 14, 2012

Happy Valentine's Day.....zawadi kwa SINGLE MOTHERS.....kutoka Homez Deco.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau wetu wote, kokote mliko, nyie ndio mnaosababisha mpaka sasa tunaendelea kuwepo, na kufanya kazi zetu vizuri na kwa uadilifu.

Tarehe 14, mwezi wa pili tumekua tukisherehekea siku ya wapendanao, naamini kila mtu anasherehekea alivyopanga kusherehekea, Sisi Homez Deco tumeamua kusherehekea kwa stail yetu.

Zawadi yetu hii ni kwa SINGLE MOTHERS TUUUU, tumetoa hiyo design ya pazia hapo juu, ni kwamba, tutakuja kupima nyumbani kwako dirisha, tutawashonea na kuja kuwafanyia fitting ya pazia kwa bei ya Tshs. 20,000/- tuuu kwa dirisha 1 yaani ni punguzo la bei  50%. Njoo na kitambaa chako, baada ya sisi kukuambia ni mita ngapi za kitambaa zinahitajika baada ya kupima dirisha zako.

Zawadi hii itaanza tarehe 14/02/2012 - 14/03/2012.

Homez Deco tunajua kua single mothers wote, kua ni vigumu kulea watoto/mtoto peke yako, watoto wana mahitaji mengi na muhimu, sasa inafika kipindi kua unapitiwa hata kudecorate nyumba yako, kwa kufanya kazi sana, ili uweze kukidhi mahitaji yako naya mtoto/watoto. sasa basi msijione mko peke yenu, jua kwamba we are in the same boat na tutakua tuko pamoja katika hili taratibu mpaka nyumba zetu zitakwisha, si mnajua inabidi ku balance kila sehemu yaani budget zetu etc.
Leo tumeanza na pazia kwa 50%, kesho kitu kingine, yaweza kua ni kupakiwa nyumba rangi, kufanyiwa garden etc. 

KARIBUNI SANA KWENYE OFA HII............
NB: OFA HII NI KWA SINGLE MOTHERS TUUU, NAOMBA TUWE WAKWELI, NA WENYE HURUMA, TUSIDANGANYANE, MAANA HII NI KATIKA KUWASAIDIA KUNDI HILI LA SINGLE MOTHERS TU,,,,, KAMA MNAVYOJUA BADO HOMEZ DECO INA SAFARI NDEFU, LAKINI IMEONA ITOE ZAWADI HII KWAO, MAANA MIMI PIA NIKO KATIKA KUNDI HILI NA NINA KILA SABABU YA KUWASAIDIA WENZANGU KADRI NIWEZAVYO HATA KAMA NI KIDOGO...... NITAKUA MKALI KIASI KWA MTU ATAKAE DANGANYA, KWELI NITAMTOA KWENYE BLOG...........


MUNGU NI MWEMA NA ANATUPENDA WOTE NA AWABARIKI WOTE KATIKA KUFANIKISHA ZOEZI HILI....


4 comments:

 1. GOOD IDEA MY DEAR KWELI JAMANI MSIDANGANYE DHAMBI KWA MUNGU.MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KIDOGO ULICHOKITOA.

  ReplyDelete
 2. Jamani, I wish ningekuwa Dar.. mi ni mjane na nina watoto watatu nilikimbia mji baada ya msiba wa mume wangu, sasa nyumbani kwangu curtain box zangu hazikuwekwa vizuri zinadondoka tu, yaani sijui nifanyeje niiwahi hio ofa, si namimi na qualify kama single mother?

  ReplyDelete
 3. Hi Kado, usijali uko kwenye hili kundi, tuwasiliane, ujue utafanya nini, inawezekana kutengeneza wakati uko mbali.

  Thanks mdau wa kwanza.....

  ReplyDelete
 4. single mothers single mothers single mothers! yeeeeeah

  ReplyDelete