Wednesday, February 22, 2012

Curtains before & after........ Kijichi Mgeninani.....kazi ya Homez Deco..... Sitting room.........After...... sasa mteja wetu kabla ya kutengeneza pazia kwetu tulimshauri abadilishe rangi na apake, cream ama butterscotch, sasa kama ninavyosema jamani taratibu unaweza, mdau wetu huyu yeye alikubali kubadisha rangi, na akasema kua ataanza na mapazia, maana alikua na harusi, so angependa mapazia yawepo,  jana ndio tumefunga pazia na leo ndio harusi, tunakutakia kila la kheri..........(RANGI YA UKUTA ITABADILISHWA NYUMBA NI MPYA NDIO WAMEHAMIA, TUTAWALETEA HUMU HUMU)..
 Asikuambie mtu jamani, ukifanya kazi yako na ikapendeza na kutoka ontime, ni furaha ajabu... hii ndio team... mie hapo nilipumzika, kazi yangu ilikua kupiga picha.....haahaha.....
 ninachompendea fundi wangu yaani anafanya kazi na anaipenda kazi yake... hakuna kuchanganyana, kazi kwa kwenda mbele....
 fundi akiweka rail....
 kwa wale wenye curtain poles, pls mkitaka decoration ama swag, pls weka rail kama inavyoonekana hapa, na sio kuweka chuma tatu..... haipendezi.....

 Haya, kazi iko hapa, marinda yakitengenezwa... Phides alifanya kazi hiyo....jamani unajua bwana, hata kama ukiwa bosi katika biashara yako jitahidi uijue kazi yako, kwani itakusaidia sana na hautakua na stress hata chembe......good work Phides...
 ukiipenda kazi yako na ku meet dead line.. siku zote ni furaha tuuu Phides weee naona smile lako.....
 Vyote vinaenda kwa vipimo.... bila vipimo ni kazi bureeee
 Wakiweka decoration, kwa kiutalamu inaitwa swag..(huu ni urembo wa juu)


 Phides akimuelekeza fundi....
 Phides & Fundi wakisaidiana ku fix pazia......
 Dinning....
 hii ni kabla hatujaweka pazia.....

7 comments:

 1. Mlivoweka hiyo pazia peke yake kabla ya hiyo swag ilikuwa imependeza zaidi. sasa sijui kitu gani kimefanya isiwe na mvuto baada ya kuwega swag!! sijui ni rangi ya nyumba au sijui ni rangi ya pazia na swag havijaendana!! mawazo yangu tu. otherwise kazi nzuri

  ReplyDelete
 2. hi ruky, ni kwamba hapo ni rangi ya ukuta ndio inayokufanya usielewe hiyo pazia, as i have said, kua rangi tutabadilisha na kupaka rangi ya cream/butterscotch. huyu mteja anajipanga kwa sasa.....

  hivyo tutawaletea muonekano baada ya kubadilisha hiyo rangi ya pink... nililiweka wazi swala la rangi mapema....

  ReplyDelete
 3. mteja anachagua design anayoipenda, na pia tunampa advice, kutegemea na rangi za nyumba yake na fanicha zake, sasa ni juu ya mteja aanze kipi hapo.....

  ReplyDelete
 4. Why usingemshauri mteja akaweka pazia zinazoendana na colour ya ukuta aliyoweka awali, kuliko kuchagua pazia ambayo haiendani then arudie kupaka rangi.. I hope zipo rangi nyingi tu za material ambazo ungemtengenezea pazia na zingependezana na that pink colour ya ukuta. Ingemsaidia mteja wako kupunguza cost ya kurudia kupaka rangi..Ni mawazo yangu tu...may be cost is not an issue to her/him. Anyway kazi nzuri kila la heri

  ReplyDelete
 5. kuhusu swala la rangi kwanini mlimshauri apake cream/ butterscotch? Inawezekana mteja yeye anapendelea rangi zengine na sio lazima tu kuwa na rangi za creams na browns ndo nyumba ipendeze? Hiyo pink kidogo inashout sana, kwani hakuna pink ambayo imefifia zaidi akapaka labda, zikawa ni rangi za pastels/ florals? Nikiangalia hizo tiles kama zinapink kwa mbali. maoni yangu binafsi.
  Asante

  ReplyDelete
 6. Homez Deco, ni wataalam wa interior design, na kazi ya interior design ni kutoa ushauri kabla ya nyumba ama ofisi kujengwa ama zikiendelea kujengwa, ila kwa huku TZ inakua ni kinyume, mtu unakuta nyumba imekwisha ndio anakuita, sasa sie tunachokifanya ni kutoa ushauri, kwamba tiles, furniture, rangi za ukuta ziendane,

  kwa case hii, ni kwamba rangi aliyoipaka hata yeye mteja hakuipenda, na ndio maana akatuita tumshauri, na kutokana na tiles zake, na furnitures, anatakiwa kuwa na neutral colors, sasa baada yahapo ndio amechagua kuanza na pazia, then atakuja rangi ya ukuta, sofa, na decorations.

  Naomba ieleweke kua baada ya kumshauri mteja, yeye ndio ameamua kubadilisha rangi, hatukumlazimisha, tungeweza pia kuweka rangi zinazoendana na rangi ya ukuta, lakini vipi kuhusu tiles? angetoa? si hasara tena kubwa........

  ReplyDelete
 7. hi dear, naomba uniwekee designs tofautitofauti za vitanda ninavyoweza kuvipata kwako, size iwe ni 5*6 au 6*6, thanks, please nisaidie haraka iwezekanavyo si unajua kibongobongo pesa haikai!!!

  ReplyDelete