Thursday, February 16, 2012

Single Mothers issue....

Anonymous has left a new comment on your post "WOMENS CELEBRATION...MARCH 3":

hi Sylvia, naipenda blog yako. Of recent umeanza kunibore na hiki kitu cha "single mothers" naomba usichangaye issue kama ni Decor stick to it. Mimi nakushauri uanzishe blog nyingine ya single mothers....
Mdau

Nimepata hii email kutoka kwa mdau wangu, naomba kuijibu, kama nitakua nimekosea mtaniambia, na tushauriane...

Hii ni siku ya wanawake duniani, ambayo waandaji wameamua kuiweka tarehe 3/3, na pia itakua ni siku yangu ya kuzaliwa, . Kwa kweli siku hii ni muhimu kwetu, na mimi ni mwanamke, na sijaona kama kuna tatizo lolote lile la mimi ku support wanawake wenzangu katika siku hii.

Sasa basi, kuna kitu kinaitwa GIVE IT BACK TO THE COMMUNITY, katika hili, kuna makundi mengi sana ambayo tunaweza kuyasaidia, sisi Homez Deco tumeamua kulisaidia kundi la SINGLE MOTHERS,(na wanawake wajane pia wamo) kwa kuanza tumeanza kuwapa 50% ya mapazia, kuanzia kupima, kushona, na kufanya fittings, na vingine vingi vitafuata, kadri kampuni inaendelea kukua...

Katika kundi hili mimi pia linanihusu, nimeona hiyo haitoshi kwa kuwasaidia, sasa basi kwa kiasi fulani najua ni jinsi gani tunavyotaabika, na kunyanyasika, na kudharaulika etc.. nimeamua siku hii ya wanawake, ninajitahidi single mothers wajitokeze kwa wingi, na pia baada ya hapo vingine vitafuata, kama kua na blog yetu, kikundi chetu, etc.mambo ni mengi sana ya kufanya ili yaweze kutusaidia sisi na watoto wetu. ROME HAIKUJENGWA SIKU MOJA......NA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA

Ndugu mdau nakuomba radhi kama unaona ninakuudhi katika siku hii ya kuadhimisha siku ya wanawake kwa style yetu sisi Single Mothers, ninaamini kwa kuanzisha kikundi chetu, tutaheshimika, na kupeana support, etc.

Homez Deco pia itakua inafanya mambo ya kijamii, maana ninaamini kufanya vitu kwa vitendo ni nzuri zaidi, na itasaidia watu kubadilika, hivyo tutachanganya mada mbalimbali ambayo haitapoteza muelekeo wa blog yetu.

Nakutakia siku njema, na ninaomba pia utu support kwenye hili.

Asante.....

No comments:

Post a Comment