Thursday, February 9, 2012

Unatandikaje Kitanda chako?Leo nimeona tuzungumze kidogo kuhusu utandikaji wa vitanda vyetu, hua unatandika kitanda muda gani? asubuhi, ama ukirudi ile jioni?

Muda mzuri wa kutandika kitanda ni pale unapoamka, kwa haraka haraka utandikaji wa kitanda unachukua muda wa dk, 3-5 tu kutandika kitanda, sasa basi, design za hapo juu nilizoonyesha, hazina ugumu wowote ule, hapo kuna kitanda kama chako, godoro ambalo unalo, mashuka, mito,  duvet na bed runner.

Tandika kitanda chako kwa kutumia shuka lako safi la kulalia, halafu linafuata shuka la kujifunika, unalikunja juu upande ule unaolaza kichwa chako robo, baada ya hapo unamalizia na duvet, ama bed cover kama unalo, maana kuna set zingine za mashuka kunakua na mashuka matatu. kama umepata set ya mashuka mawili hakuna neno, utalikunja hilo shuka upande wa juu robo, maliza kwa kupanga mito yako kama iko miwili, minne, etc.

Upande wa chini inapolala miguu, tupia bed runner, iendane na foronya, hii sasa unaweza tupia kwa juu ya kama inavyoonekana katika picha za hapo juu.

Natumai somo limeeleweka, tutumie email kwa maswali zaidi. somo lijalo nitawaeleza aina ya mito na size.

1 comment:

  1. Devine! Soo beautiful,i am using your tips to teach my little girl to make her bedroom tidy and relaxing. Be blessed.

    ReplyDelete