Monday, February 20, 2012

Haya, hii ndivyo ilivyokua kwenye interview na capital radio leo......



Interview ilikuanza saa sita mchana, na nilihojiwa na Sara, ilikua ni kuhusu kupamba living room yenye space ndogo, so maelezo yakawa kama yafuatavyo....

Katika kupamba living room yenye space ndogo, kwenye upande wa rangi inatakiwa tupake rangi, zilizoko kwenye group ya cool colors, ambazo ni Blue, green, violet ziwe light. rangi hizi zinafanya chumba kidogo kua kikubwa,

Kwa upande wa fanicha, hapa inabidi tuweke fanicha ambazo ni mult purpose, nikiwa na maana kua kama ni tv shelf, liwe linaweza kuweka magazine, tv, vyombo kiasi etc, ukija kwenye sofa ni L-shape pekee ndio itakayopendeza hapo, stools zile za sets, yaani zinakua zinaingiliana, kama mnazijua zinakuaga ni 3 size tofauti.   

Carpet, unaweza kuweka wall to wall carpet, ama kama kuna tiles, basi weka carpet za round, ama pembe nne etc, ziwe ni ndogo.

Tukamalizia na mapambo, kua weka picha za ukutani za wastani, kama ni 1, ama kama ziko tatu basi zipange vizuri zikifuatana.

NB: kuna kitu tunakiita Focal point kwenye interior design & landscaping, maana yake ni kua, ni kitu chochote kinacho attract macho cha kwanza kukiona uingiapo mahali. sasa yaweza kua ni garden, picha za ukutani, pazia, sofa, music system etc.

Nawashukuru sana Sara na Hawa wa Capital Radio kwa kunipa chance hii ya kuongea na watanzania wenzangu na kuwaelekeza nini cha kufanya na living room zao........

Na hapo ndipo tulipoishia,..... nitawajulisha ni lini tena tutaendelea na mafunzo haya.........Capital Radio......

5 comments:

  1. Hi Ms. Namoyo! I stand to be corrected, why do we have to put vyombo in the living room kwenye TV shelf/cabinet? To me that's unaacceptable, labda mie ndio mshamba! Otherwise good job na ahsante kwa kutuelimisha!

    ReplyDelete
  2. hi mdau, kuweka vyombo katika tv case ni kwa wale wenye living room ndogo, huwezi kuweka tv case, na kabati la vyombo hapo hapo, ndo maana nikasema vitu vinavyotakiwa kukaa hapa ni viwe multpurpose, kumbuka huyu mtu hana dinning room.

    na makabati ya hivyo yapo, nimeogelea kwa wale wenye living room ndogo, na hawana dinning room. kujaza makabati space itazidi kua ndogo nani uchafu

    asante mdau,natumai umenielewa.

    ReplyDelete
  3. habari mama jaydan, mi nauliza tu, nina chumba na sebule tu ndoo za maji naweza kuweka sebuleni au chumbani? asante natumai umenielewa.

    ReplyDelete
  4. habari ndugu mdau, sasa nataka kujua kua hiyo nyumba mnakaa wengi ama inakuaje? lakini pia ningekushauri, ndoo za maji zikae nje... maana nategemea ndani una fanicha, sasa ukiongeza na ndoo za maji kutakua hakuna mpangilio mzuri....na vyumba vyetu navijua vilivyo vidogo.....

    karibu.

    ReplyDelete
  5. asante kwa kunielewesha
    , hiyo nyumba naishi mimi na mume wangu tu.
    Mdau

    ReplyDelete