Friday, February 19, 2010

Prayer room in your house



Jana nilipokea Email kutoka kwa mdau wangu aitwae Lucy au Mama P. Na hii hapa ni Email yake: Hi Sylivia!

Natumai mzima, pole na majukumu.

Sasa mimi mdada yule wa zile resting shelters ambazo ulijitahidi ukanitafutia nzuri.
leo nakuomba unisaidie hivi unaandika vitu vingi nafurahia sana ukiwa kama mkristu mwenzangu hivi chumba cha kusalia kwenye nyumba zetu inakuwaje hili swala naona kila mtu anaweka library tunajisahau na hili ikifika usiku tunasali sitting room hapo tunafoge tu au vp wenzetu nchi zilizoendelea nyumbazao vp nao? tunakumbuka chumba cha wageni wkt unaweza kukaa mwaka mzima usipate hata huyo mgeni jamani waelimishe watu ni muhimu sana walitambue hili nalo.

Asante,.
Mama P!

Kwa kweli hii prayer room nilijisahau, ila namshukuru sana sana, kwa kunikumbusha, na ndio maana huwa ninapenda sana maswali, na kujadiliana na ushauri kwani ni kwa faida ya wote.

Chumba hiki waweza kukitengeneza kulingana na Nafasi ya hicho chumba na idadi ya familia yako au watu watakao kuwa wanakitumia.

Naomba msinishangae kwamba nimewaletea ya Kikristo tuu, hapana naendelea kuandaa na ya ndugu zetu waislam kwani mie asili yangu ni muislam ila nilibadilisha dini na kuwa mkristo kwa kumfuata mama yangu. Nampenda sana,

1 comment:

  1. habari Dada Sylivia
    Napenda kuungana na Mama P. ni kweli chumba cha kusalia ni muhimu katika nyumba( kwa dini zote) kweli sebuleni kuna shughuli nyingi zinazoweza kukufanya ushindwe kutenga muda wa kusali,kwa wale mnaojenga sasa au mliokwisha jenga ni vizuri mkaangalia uwezekano wa kutengeneza chumba cha kusalia. Mi nimeshaweka!
    Asante Mama P kwa kutukumbusha
    Mama C

    ReplyDelete