Tuesday, February 16, 2010

Mpangilio huu umekaaje?2 comments:

 1. hello dada Wa Homezdeco.Mi napenda sana kusoma hii blog yako!ina vitu vzr!Tatizo ninaloliona hapa,unaweka au unazungumzia sana vitu ambavyo ni standard ya juu.Sio huu urembo hapa tu,bali vitu karibu vyote!Sisi watanzania tulio wengi maisha yetu ni ya kawaida sana bado!hatuna mijumba ya ajabu,tuna sitting rooms za kawaida,tunaaford mapazia ya kawaida..fenicha simple.etc!Tuoneshe hizi arrangements mbalimbali kwa kutumia vitu hivi tulivyonavyo.Unakuta umeweka mijumba ina fenicha za hali ya juu,kiasi kwamba mtu wala hajishughulishi kuiga namna ya kuweka hayo mapazia kwa mfano!piga picha nyumba zetu hizi hizi,na mapazia yetu haya haya,na makochi na meza zetu za middle class.Zitatusaidia.Au labda hii blog yako umetarget watu wa class ya juu mwaya!ila km ni watanzania wa kawaida,tuwekee na zinazoendana na class yetu.changaya changanya!Mi binafsi nabakiaga Kuangalia tu!

  ReplyDelete
 2. Habari yangu nzuri namshukuru mungu kwa kila kitu, nashukuru sana kwa comment yako, kwani ninapopata comments huwa ninafurahi sana huwa ndio msingi wangu wa maendeleo.

  Kwenye hii blog site yangu, lengo ni kuelimisha jamii na kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine, na nime base kwa watu wa hali za kimaisha za watu wote.

  Naomba kukufahamisha kuwa kuna msemo usemao cheap is expensive. Mimi ninajitahidi kuwaelezea na kuwaonyesha wenzetu (nchi zingine) wanafanyaje na wanaishije ili upeo wa akili na fikra kwenye upande wa decoration ukue.

  Mimi nimekuwa nikitoa makala mbali mbali, na picha mbali mbali ninazofanyia kazi kabla ya kuzitoa kwenye blogsite, na ninapenda kuwafahamisha kuwa vitu ninavyoviuza havina gharama sana kama mnavyofikiria, tumekuwa na uoga wa kutembelea maduka. Fanya window shopping usiogope. Wenzetu kila mwaka wanabadilisha fanicha, etc majumbani mwao. Na sio kwamba wote wana hela, ni kujipanga tuuu.

  Chukulia mfano mmoja tu ninaotaka kukupa, ni watanzania wangapi (BAADHI YAO SIO WOTE) ambao wako radhi kubeba simu za gharama, kuvaa nguo za gharama etc, lakini kutoa hela kununua kitanda, ama mito ya kwenye makochi yake anaona ni ghali. Nina amini msemo huu kupanga kuchagua.

  Pia ninapotoa picha kwenye blog hii sio lazima ukaiga kila kitu, chukua aidia, kumbuka kila siku nasema tuwe creative. DO NOT COPY AND PASTE kwenye hili swala la decorations. JUST COPY EDIT AND PASTE halafu uone kama umetumia hela nyingi.

  Nakutakia siku njema

  ReplyDelete