Monday, February 15, 2010

Hizi picha nimetumiwa na mdau wangu,Sis Rehema ila sasa amekuwa kama dada yangu kwa jinsi tunavyo wasiliana mara kwa mara, na kumfanyia kazi zake.

Nimependa hii sitting room arrangment, rangi ya ukuta pia imetulia, mpangilio ni mzuri na inavyoonekana mwenye nyumba hiii ni mpenda sana decorations.
Last week niliongelea hii design ya meza, na inaweza ikawa ina kioo kimoja kikubwa ama ukaweka vioo vidogo kama alivyoweka yeye, na namshukuru sana dada yangu Rey, kwa kunitumia picha hizi, meza hii waweza kuweka decos, kama alivyoweka, ama ukaweka upande wa koridor, ama karibu na mlango ukawa unawekea vitu vidogo vidogo kwa muda mfupi.

It's all about the bedroom wapendwa wangu, kwani nusu ya maisha yako humalizia hapa, sasa ukipadharau, ama kupaweka pachafu, kwanza utaumwa, na hutopenda kulala humo ndani kila mara utakuwa unapakimbia nyumbani kwako, si aibu hiyo?
Arrangment ni nzuri, picha ukutani zimekaa kwa kupangiliwa, tv nayo iko mahala pake, kwa ufupi chumbani hakuhitajiki makorokoro mengi.
Hapa pia ni chumbani upande wa dirisha, huwa kunakuwaga na vile viti vya kukalia wakati unavaa viatu, nilisha vizungumzia last week, yeye huyu kaamaua kuweka upande wa dirishani kwani space yake haitoshi, na imependeza sana, ona rangi zake zilivyotulia, mapazia simple and nice.
Hapa ni nje, wengi wetu tunasahau kama sio kupadharau, weka viti vyako viwili, sio lazima vya wageni hata wewe ukihitaji kupumzika basi hapa hufaa.

All in All, nakushukuru sana Sis Rey, and I wish you all the best sis, na endelea kutupatia picha zaidi zaidi ili tuendelee kuelimishana.

2 comments:

  1. Nimependa hiyo meza ya kuwekea pics na kioo ukutani waweza kutengeneza kwa shs?

    ReplyDelete
  2. Meza hiyo inawezekana, ila tutaifanyia modification, badala ya mbao tutaweka kioo. bei ni tshs. 290,000/= karibu

    ReplyDelete