Monday, February 8, 2010

LEO HII NAZUNGUMZIA USAFI WA MAJUMBANI KWETU KWA UJUMLA

HATA MITAANI TUNAPOISHI, TUNZA LINDA MAZINGIRA NAYO YATAKULINDA
WANA JAMII, Hili suala la usafi wa majumbani kwetu tunapoishi na familia zetu, ni la muhimu sana, hata sehemu tunazofanya kazi, usafi unaitaji ushirikiano mkubwa sana, ktk familia, maofisini, masokoni, na sehemu za biashara, kwa ujumla wanajamii wenzangu lazima, muelewa usipotunza mazingira yanayokuzunguka, matokeo yake ni milipuko ya magonjwa, na kuambkizana hii inakuwa sehemu za biashara migahawa, mahotelini, madukani, sokoni kwa kina mama lishe na baba lishe tukumbke suala la usafi wa vyombo tunavyotumia, kuonya na maji ya moto, na tusitumie vyombo vya plastics, na kama tuna vitumia vioshwe na maji ya moto, usafi kwnye mkusanyiko wa watu pia na wanapopata huduma, sio, kuna baadhi ya sehemu wanatoa huduma za chakula, kumezungkwa na uchafu, basi panya, mende, buibui, mavumbi, jamani watumiaji wa huduma hizi ukiona sehemu siyo safi usiende au mwambie mhusika,maana.magonjwa hayatatusubiri,kila mtu awe mulinzi wa afya yake.

From Mrs. Jossanne

1 comment:

  1. Dada umeongea kweli. maana kuna watu hawajali kabisa usafi wa maeneo yao. tena na mvua ikinyesha ndo kwanza wanafungulia na vyoo vyao kukwepa gharama ya kuvuta maji machafu. na kutupa viroba vya uchafu kwenye madirisha ya watu. looh inasikitisha na inatia kinyaaa!

    ReplyDelete