Monday, July 23, 2012

Kazi ya Homez Deco site ilikua Mabibo...(www.homezdeco.co.tz)

 Kitanda baada ya kufunga.... hakijatandikwa bado........
 Kitanda kimeshafungwa....pamoja na bedside table zake
 Shoe rack ya pea 20
 Nilipenda rangi alivyopaka ukutani

 korido..... angalia rangi zilivyochanganywa......
Kazi ya homez deco katika nyumba hii ilikua ni fanicha za chuma, ambapo ni set.....kitanda, dressing table, bedside 2, shoe rack.....

Nilichokipenda katika nyumba hii ni mpangilio wa rangi, nyumba ni ndogo, na mpangilio wa rangi ni mzuri, siku zote jamani, vyumbani tusipake rangi ambazo ni kali... kumbuka chumbani nisehemu ya kulala, kupumzika, sasa unapopaka rangi kali, hata kichwa chaweza kukuuma,,, na ukashindwa kujua nini kumbe tatizo ni rangi ulizozipakaa ukutani kwako.

Chagua rangi unayoipenda, na kama rangi ni ya giza paka ukuta mmoja ama kuta mbili, halafu zilizobaki, paka rangi ambayo yenye kuleta mwanga...

Mfano mzuri ni nyumba hii... angalia alivyochanganya rangi..........yaani kweli kabisa, ukipumzika,,, unajisikia kabisaaa. kwamba umepumzika,  inawezekana kabisa ukadecorate mwenyewe na nyumba ikapendeza..... jiamini.....

tulimshauri pia pazia azipunguze urefu, maana pazia hazitakiwi ziburuzike......

waweza pia wasiliana nasi kwa ushauri zaidi....

Nashukuru kwa mdau wangu huyu.....

 may God be with u.....

No comments:

Post a Comment