Wednesday, July 25, 2012

Nyumba yako iko mikononi mwako........



Sisi ndio waamuzi wa nyumba zetu tunataka ziweje.....

Muonekano wa nyumba yako ndio unaokuonyesha wewe ni mtu wa namna gani.....

Na kumbuka nyumba inatakiwa ikukaribishe, na sio ikuchukize....

Iwe ni ya kupanga, ni yako umejenga etc... hiyo ni yako... tumekua na mazoea,  kama si maono ya kwamba, nyumba ya kupanga si yangu sasa siwezi kuipamba mpaka nipate yangu....

Jamani haya yamepitwa na wakati..... nyumba unayoishi ni yako na ndio hapo uishipo, sawa.... kuna ile ukifanya ukarabati mkubwa mwenye nyumba anakutafutia visingizio, kama si kukupandishia kodi basi, hatokuongezea mkataba atataka uondoke....

Sasa basi leo ninakuja na ushauri wa nini ufanye na ambao sio gharama kwa kuremba nyumba yako...

Katika nyumba yako hiyo uishio, unaweza ukaipamba kwa vitu vinavyohamishika.. yaani fanicha, mapambo, pazia nzuri, chuma za pazia nzuri. rangi za ukuta ukiwa ni mtunzaji mzuri kuna rangi za maji, yaani sio wash n ware......na kuna rangi za acrylic,ziko za makampuni mbalimbali...

Jaribu pia kubadilisha badilisha mpangilio wa fanicha, kukarabati, kama kuna vitu vimeachia virekebishe usisubirie mpaka viharibike kabisaa.... na pia jaribu mara kwa mara kufanya usafi kwa kina...... hii husaidia sana kuona nini cha kutoa, na nini cha kubaki....

Tusisahau pia kwa upande wa garden. kuna msemo usemao kua "first impression is the last impression"

ukiotafakari msemo huu utakubaliana nami.......

Uamuzi ni wako.. na kumbuka rahisi ni gharama siku zote, maana havidumu.....

No comments:

Post a Comment