Tuesday, July 17, 2012

Introducing Candra Saloon.........(Wanawake tuko juu sasa.......)

Tuko kwenye pozi .......
 Nikiwa najiandaa kuanza kutengenezwa......
 Nikitengenezwa.........

 Kucha zangu tayari sasa........
  Her name is Rahma- Owner of Candra Saloon - 0712 - 007077


Candra saloon iko kinondoni, pembeni na barclays bank kuna ghorofa, saloon hii iko hapo...... Ninachokipenda kwa sasa asilimia kubwa ya sisi wanawake tuko juu tunajishughulisha kwa kufanya kazi na biashara, hatuna uoga kama zamani, ama tunasubiria tuuu tuletewe hela....

Saloon hii kinachonifurahisha ni usafi, na huduma zake..... nimependa pia mwenye saloon alivyoweza kupamba saloon yake, na kutumia space vizuri, kwani kabla ya kufanya kitu, ni lazima ujue ukubwa wa sehemu yako, na nini uweke na nini usiweke...

Hauhitaji kua na space kubwa, ndio biashara ionekane, kila mtu anafanya biashara kulingana na uwezo, sasa kwa baadhi, ya watu bado wana ile dhana kua, mpaka kitu kiwe kizuri ni mpaka pawe pakubwa, ama barabarani etc.......

Kinachohitajika ni huduma nzuri, kazi iwe ni nzuri. etc. ukiwa na hivi vyote, basi kokote uliko utafikiwa, tusiogope kufungua biashara eti nani atasema nini ama atasema vipi.........

Hii ndio saloon wananitengeneza kucha zangu, kwa kweli mwanzoni nilikua sina mawazo ya kucha..... lakini walinifanya nimeanza kupenda kucha zangu na kutengeneza.

Service zao ni nzuri, kingine ni kwamba, ukiwa unataka kupaka rangi ya miguuni, basi wanakusafisha kwanza. sio kama baadhi ya saloon zingine, hua wanakufuta, tuu rangi halafu wanakupaka, hapa wanakuosha ndio wakupake,.....

Na pia ukipenda wawe wanakukumbusha appointment yako ya kucha wanafanya hivyo...

Karibuni sana sana.... na bei zao ni nzuri tuuuuu.....

2 comments:

 1. Kwa kweli Sylvia Hujakosea,mi pia nawakubali sana kwa usafi,huduma n.k.

  Hongera sana Rahma,Hongera na Sylvia kwa kuona na kusema ukweli daima.

  Kind regards
  Myah - weddingspottz.blogspot.com

  ReplyDelete
 2. KWA KWELI HUJAKOSEA, HATA MIMI NIMEFIKA HAPO SALON TENA NILIKUWA NAKWENDA SALON NYINGINE NILIYOZOEA KWENDA JIRANI NA HAPO TENA MAARUFU, NIKASEMA NGOJA NIINGIE KUTENGENEZA KUCHA NA NYWELE ZANGU HAPO CANDRA SALON.YAANI NAKUBALIANA NA WEWE 100% KWANZA WAKARIMU,WANAKUSHUGULIKIA VIZURI NA OTHER INTERTAIMENT, NA NIWASAFI SANA. MPAKA LEO NDIO SALON YANGU TENA MIMI NA MUME WANGU, HUWA ANAPENDA SANA KWENDA KUFANYA PEDICURE. NA WALA SIHAMI HAPO HATA SIKU MOJA,KWA KWELI WAPO JUU SANA, HUYO DADA PONGEZI ZAKE NAMPA NI MBUNIFU SANA. ALAFU NI BINTI MDOGO TUU. HONGERA SANA BINTI

  ReplyDelete