Monday, July 16, 2012

Pazia.......


Naomba kuchukua nafasi hii kwa kutoa elimu kwa upande wa pazia... wengi wetu tunazijua pazia na umuhimu wake ndani ya nyumba, zetu ama ofisi zetu...

Pazia kuna design nyingi tuuuu, ingawa kwa kuanzia inategemea umeweka nini ya kushikia pazia, ama unataka kuweka nini ya kushikia pazia zako.

kwanza kuna
curtain poles
rails
curtain box.

sasa unachagua ipi kwa ajili ya pazia zako? ukishajua ndio sasa uje kwenye pazia, na design hizi zote ni nzuri tuuuu... ni wewe uamuzi wako.

ukija kwenye pazia yenyewe sasa... raha ya pazia na ipendeze, pazia inatakiwa ijae kwenye dirisha ndio itakaa vizuri na kupendeza....

kwa mfano, dirisha la mita 2 linahitaji kitambaa cha pazia nzito mita 5-6 na hesabu hii inakwenda sawa na pazia nyepesi.... sasa basi utapata kua dirisha moja linahitaji mita 10 - 12 jumla. na hii ni kwa design za kawaida zisizo na marembo......raha ya pazia ijae kwenye dirisha.... ndio inapendeza......

kwa huku kwetu bitambaa vizuri na bei zake ambazo ni za kawaida mita moja inaanzia tshs. 15,000/-......na kuendelea...

na kuna vingine mita moja inaanzia tshs, 80,000, 150,000/- na kuendelea sasa ni uwezo wako tuuuu wewe,,,, na vyote vikishonwa vinapendeza.... sana.... tofauti ni ubora wa kitambaaaa,,,, na mapambo yake.....

hizi gharama nilizozitaja hapo ni za kununua vitambaa pekeee......

na sisi kampuni yetu homez deco, tunaanzia kushona kwa dirisha 1= 35,000/- design ambayo ni simple... na bei zetu tunakuja kukufungia mpaka nyumbani kwako(usafiri ni wa mteja), haijalishi unakaa wapi, hata mikoani tunakuja kukufungia ni maelewano tuuuu.....(kwa wale ambao hawana muda wa kuzunguka madukani, tunatoa huduma ya sisi kufanya kazi yote bila malipo zaidi.....ya kukutafutia kitambaa, kushona, na kuja kukufungia...)

Pazia ni gharama hilo naomba lieleweke lakini pia inategemea na unanunua kitambaa cha bei gani design gani unataka?..... na ukiweka pazia nzuri na yenye ubora.... unaweza ukakaa nayo kwa muda mrefu.....

Ninapenda kuwakaribisha wote ofisini kwetu kwa huduma bora, na kwa kazi nzuri kama zinavyojionyesha...

na sasa niko mbioni katika kuboresha huduma zetu kwani sasa soko limekua, na nina kila haki ya kumshukuru Mungu wangu kwa kila anayonitendea.....

Nawatakia siku njema......

No comments:

Post a Comment