Chumba ni kile kile, furniture ni zile zile ila tumecheza na rangi tuuu, na kumebadilika. Utakubaliana na mimi kua kupaka rangi kuna badilisha muonekano wa sehemu kabisa. Brown ni rangi ambayo imetulia, hivyo tumeamua kuichangamsha kidogo.
Hapa kama unavyoona, zimetumika rangi tatu, brown ambayo ni makochi, na blue ambayo ni accessories, nikiwa na maana ni mito, puff hiyo ya katikati, throw iko juu ya puff, na white ambayo ni taa ama lamp shade, maua, na kwenye pazia pia kuna white, bila kusahau carpet. Sasa tumejionea kuwa rangi hizi zikitumika ama kuchanganywa zinapendeza kweli.
Hii hapa tumetumia rangi rangi tatu, brown ambayo ni makochi na puff, na kidogo iko kwenye carpet na mapazia, kuna white ambayo ni taa (lampshade
Hapa napo tuna rangi 5. Rangi hii ni peach, imetumika ukutani, mito, throw, na kidogo kwenye carpet, brown iko kwenye makochi, puff, na kwenye tray ni dark brown, maua yana red na kuna kama kiurembo kwa mbali kwenye stool ya taa ni red pia, ukiangalia taa ni white, flower vace ni brown, na cream pia imetumika kwenye curtain box, na kwenye mto pia imechanganyika brown na cream kwa mbali, bila kusahau carpet pia.
NB: Kila rangi inayotumika kwenye ku decorate inahesabika(sasa sijajua kiswahili fasaha hapa),
hata kama ni kidogo kiasi gani, na kama mlivyoona hapa, chumba hicho hicho unaweza kucheza nacho kwenye rangi tofauti tofauti na kukapendeza. Hata njano ingefaa, orange ingefaa any color ingefaaaaa ni upangiliaji wako tuuu ndio utakaofanya paonekane pazuri, ndio maana nawaambia TUACHE UOGA WA KUCHEZA NA RANGI. JUST BELIVE IN YOUR SELF.
Nawatakia weekend njema.
No comments:
Post a Comment