Tuesday, April 13, 2010

Imeshawahi kutokea kua una ipenda nyumba ya mwenzio kuliko yako? kwa upande wa rangi aliyoipaka nje ya nyumba yake? Exterior paint



Kuna nyumba jamani hapa kwetu yaani ukiiona una admire kweli kwa jinsi rangi zake zilivyopangiliwa kupakwa, Kuna msemo mmoja hua unatumika sana kwenye industry ya hotel unasema FIRST IMPRESSION IS THE LAST IMPRESSION.

Msemo huu una maana sana sana, na ukiuzingatia huu msemo utakusaidia katika kila nyanja. Mimi sioni mantik/maana, kua unapendezesha nyumba yako ndani halafu nje kumeoza, haileti maana kabisa, huo nauita ni uchafu.

Rangi za nje siku zote ni tofauti na rangi za ndani, kwani rangi za nje zinakua ni maalum kwa kuweza kukabiliana na hali ya hewa yoyote ile, na inahitaji uwe ni muangalifu ili usije ukachanganya wakati wa kununua.

Kuna wengine wanapenda kupiga chuping kwenye ukuta wa nje, na wengine wanapiga rangi, yote hii ikipangiliwa vizuri inapendeza sana. Na naomba ijulikane kuwa hata chuping kuna za rangi, sio tuu ile rangi ya kaki tuliyoizoea.

Kwa ushauri tuwasiliane,

No comments:

Post a Comment