Tuesday, August 18, 2009

vitu vinavyohitajika jikoni

Ndugu wasomaji, mtakubaliana na mimi kuwa wengi wetu huwa hatuna katabia ka kubadilisha vitu vilivyochakaa vya jikoni. Utakuta jikoni kwa mtu kuna vitu vingi kweli lakini vinavyoweza kutumiwa ni kidogo mno vingine vimechakaa na vingine vimeharibika lakini mtu kakaa navyo vya nini jamani. Usivyotumia gawa vilivyoharibika wape wanaonunua scepa. Ninachoweza kushauri ni kuwa jipe ratiba yako kwa mwaka kama itakutuhusu kubadili vitu mara 2-3 sio vibaya. Ila kwa sie wengine basi japo mara moja jamani.

Jinsi ya kujua ni vipi waweza kubadilisha vitu vilivyochakaa jikoni kwako:

  • Toa vitu vyote vilivyochakaa
  • Viorodheshe kwenye karatasi
  • Angalia vitu utakavyovitumia
  • Kanunue na kuviweka ndani

Ni rahisi ama sivyo jamani, na sio lazima viwe vya ghali angalia mfuko wako.

Kujaza jiko vitu vilivyochakaa jamani haipendezi. Tuwe na tabia ya kubadilisha jamani

No comments:

Post a Comment