Monday, August 17, 2009

Jinsi ya kukarabati jiko kwa bajeti ndogo

Uta kubaliana na mimi kuwa hata kama nyumba yote ni nzuri, lakini watu huishia jikoni, sasa basi kuna njia nyingi ya kukarabati jiko lako bila kuchukulia mkopo.

Kwanza jua jiko lako linahitaji nini kwa ujumla.

  • Makabati yako yanahitaji ukarabati?
  • Je sakafu inaendana na jiko?
  • Mazingira ya jiko kwa ujumla yako sawa?

Kama haviko sawa ama viko sawa basi kuna vimatatizo vidogo vidogo tuu, Jua ya kuwa kwenye jiko kuna sheria moja huwa tunaiita ni PEMBE TATU.

Nikisema pembe tatu nina maana ni:

  • Sinki
  • Friji
  • Jiko

Sasa basi vitu hivi vyote visizidiane futi 9 ama pungufu ya futi nne inategemeana na ukubwa wa jiko. Hizi pembe tatu zisiingiliwe na vitu kama makabati na flow ya vitu.

Kwa upande wa makabati kama yana hali nzuri sio lazima kubadilisha, paka rangi milango na badilisha vitasa vya makabati.

Upande wa meza ya kutayarishia vyakula, sasa hapa inategemea na uwezo ila waweza weka fomaika, mable, ama mbao na ukaipolishi vizuri na pakaonekana super.

Naomba kuwakumbusha kwa upande wa sakafu, jikoni hakutakiwi kuwa na sakafu inayoteleza.

Vitu nilivyovitaja hapo juu vikiwa haviwezekani kwa baadhi yetu basi kuna njia m badala, paka rangi jiko lako kwa rangi zenye mwanga zaidi.

Taa nayo bila kusahau, weka taa yenye mwanga wa kutosha

NANI KASEMA JIKO LINATAKIWA KUWA NA RANGI NYEUPE?

KUWA MBUNIFU - INAWEZEKANA HICHO NDICHO CHUMBA UNACHOKITUMIA MUDA MWINGI.

Have fun!!!!

1 comment:

  1. Jamaniiii naipenda hiiii blog.Sylvia you are a star kwa kweli.

    ReplyDelete