Wednesday, August 26, 2009

Dizaini za Mapazia

Leo nimependelea tuongelee kuhusu mapazia. Kwenye sekta hii kidogo kuna ka ugumu kwani watu wengi huwa wanadhani ilimradi pazia tuuu. Mapazia yalianza kutumika tokea karne ya kumi na tisa. Nia ya mapazia kwanza ni kuzuia mwanga wa jua kuingia ndani, vumbi, na kuzuia watu wa nje wasione ndani wakati wa usiku na kupendezesha nyumba etc.

Mapazia yanaweza kupendezesha nyumba ama yanaweza kuharibu muonekano wa nyumba. Naomba kuwakumbusha kuwa kuna mapazia ya aina 2. Mepesi na Mazito. Muangalie na Texture ya mapazia.

Mapazia yako yaliyotengenezwa kabisa na kuna ya kuchagua kitambaa kikashonwa.

Sehemu za baridi ni vizuri kuweka mapazia mazito na za joto weka mepesi. Nikisema mepesi sio yale ya kuanganza ndani bali vitambaa vyake vinakuwa sio vizito sana.

Kwenye dirisha kunatakiwa kuwe na mapazia mawili, jepesi linalosaidia kuzuia vumbi ndani, na la kawaida liwe zito zito kiasi kama ni kwenye joto na baridi liwe zito.

Kwa upande wa rangi ya mapazia jitahidi rangi ziwe zinashabihiana, kuna yaliyo na marembo na mengine hayana urembo wowote.

Sasa kuna dizaini nyingi sana za mapazia, yaweza kutumia katein boxi,  vimbao vidogovidogo vya curtain poles nisaidieni kiswahili, kuna ya mbao zinazofunguka, aluminium etc.

Tengeneza mapazia kutokana na dirisha lako lilivyo. Madirisha ya jikoni, stoo, ofisini na chooni ni vizuri ukaweka mapazia mafupi. Kuliko baki weka mapazia marefu na weka kambaa mahususi kwa kufungia pazia au vichuma vinavyogongewa ukutani vya kufungia wakati wa mchana.

Vipimo pia jamani vinamata hapa usiweke pazia mpaka likaburuza chini.

Kuna dizaini za mapazia ya nyumba kubwa na nyumba ndogo, msichanganye hapo maana nyumba itaonekana kituko.

No comments:

Post a Comment