Tuesday, August 25, 2009

Meza za chakula

Habari za muda ndugu zanguni, Leo nimeonelea kwenda kwenye meza za chakula. Hapa kama mnavyojua ni sehemu ya kupata mlo baada ya kupikwa vizuri na kwenye sehemu safi tena kwa usafi. 

Jambo la kwanza kabla hujaamua kuweka meza ya chakula nyumbani kwako, angalia kama kuna nafasi yakutosha kuweka meza ya watu wangapi. Sasa usije weka meza ya watu sita kumbe nafasi ni ya meza ya watu wa 4. Nafasi ni muhimu sana

Wengi wetu tumezoea kuweka vitu vingi saana mahala hapa. Kuweka vitu vingi sio kupamba, weka vitu vichache na bado kutaoneka kuzuri tuu. Pia kuna mazoea fulani hivi utakuta mtu anavyombo vyake vizuri tuuu kaviweka kabatini, na yeye anatumia vyombo tuu vya kawaida au vimechakaa na kuchakaa, ukiuliza utaambiwa hivyo ni vyombo vya wageni. Jamani hivi kweli ni inaingia akilini maana wewe mwenyewe umekwenda kuvinunua na huvitumii.

Tusiwe na hako katabia, tumia vyombo vyako ulivyonunua wewe mwenyewe au hata kama umepewa zawadi.

Usafi pia ni muhimu, usipojaza vitu vingi, itakuwa rahisi kwako kufanya usafi. Kumbuka kuwa dasta ya kufuta meza ya chakula iwe ni ingine, na ya kufuta mavumbi iwe nyingine. Mimi huwa nina penda mtu atumie dasta za rangi nyeupe kwa kufutia meza kwani hicho ndicho huonyesha uchafu kwa urahisi. 

Hakikisha muda wote meza yako ni safi waweza pia kuweka mapambo, kama vile matunda ya atifisho, maua ya atifisho ama fresh, mishumaa. Na kuna vitambaa ambavyo ni vyembamba na nivirefu kutegemea na urefu wa meza yako. Vinaitwa Table runner sa sijui kwa kiswahili vinaitwaje nisaidieni, havifuniki meza yote. 

No comments:

Post a Comment