Monday, August 31, 2009

Jinsi ya kuning'iniza picha za ukutani

Picha za ukutani ziko za aina nyingi sana, na wengi wetu tunapenda sana picha mie mmoja wapo. ila wengi wetu hatujui jinsi ya kuzi ning'iniza picha hizo kwani utakuta ukuta una matundu matundu ya misumari ndio ujue hapo kazi ya picha ilikuwako.

Kuna step 4 za kufuatwa kabla ya kuning'iniza hizo picha na haijalishi ni picha gani wadau wangu. Vitu vinavyohitajika ni:

  1. Penseli
  2. Karatasi
  3. Nyundo, drill
  4. Misumari ama hook za ukutani

Steps:

  1. Kwanza angalia ukuta wako ni wa aina gani ili ujue kama utatumia grill ama nyundo, halafu chagua ni sehemu gani ya ukuta unataka kutundika picha zako, Picha kubwa huonekana vizuri kwenye ukuta mkubwa(sehemu ya ukuta pawe pakubwa), na picha ndogo huonekana vizuri kwenye ukuta mdogo na ni vizuri ziwe picha mbili mpaka tatu yategemea na sehemu ya ukuta wako. ( sehemu ya ukuta pawe padogo) 
  2. Hakikisha una ning'iniza picha zako usawa wa macho, isiwe juu ama chini. Picha kubwa zaidi hupendezea kutundikwa juu ya sofa ama sehemu ya kuwashia moto sitting room kwa wenzetu walio sehemu za baridi.
  3. Chagua picha unazotaka kuzining'iniza ni vizuri ukizichagulia sakafuni, halafu kata karatasi usawa na hizo picha, chukua penseli yako na hiyo karatasi nenda ukutani jaribishia ukiona iko sawa basi weka alama na penseli yako, chukua hook ama misumari pigilia tayari kwa kuning'iniza picha zako.
  4. Kuning'iniza picha za group, zisambaze sakafuni, chagua na jaribu kuzipanga kubwa kwa ndogo ama ndogo zote na angalia ukiona umeridhika na muonekano wa picha hizo, basi fuata stepu hizo 3,kwa wale wenye nyumba za ghorofa tundika kwenye ngazi, pia yapendeza. Na utakuwa umependezesha nyumba yako na HAKUTA KUWA NA MASHIMO MASHIMO.

No comments:

Post a Comment