Monday, November 26, 2012

Wallpapers...Available @ Homez Deco...



Wallpapers ni karatasi za urembo ambazo hubandikwa ukutani. Waweza bandika ukuta mmoja ule wa tv kwa sebuleni na chumbani ule ukuta ambao hauna madirisha.....

Wallpapers, inatakakiwa kubandikwa kwa uanvalifu mkubwa, maana inabidi ukuta uwe ni mzuri na msafi yaani usiwe na mchanga mchanga,

Homez Deco tunakuja kukubandikia sisi wenyewe, ukinunua....

Kwa hesabu za haraka haraka wallpapers zinaweza kuingia kwenye ukuta mmoja kuanzia mbili mpaka tatu, inategemea na ukubwa wa ukuta wako.....Hivyo utakapochagua tunapima ama utapima urefu na upana ili kujua tunapata square meter ngapi, ndio tupate idadi zinaingia ngapi....

Kumbuka muda ni mchache kuelekea sikukuu,
Karibuni .......

6 comments:

 1. Hi,naitwa angela ninapenda blog yako coz huwa ninapata ideas nyingi nzuri kwa kuboresha nyumba yangu.ninaomba unisaidie namna ya kujiunga gnld au kama unaweza niunganisha na mtu ambaye atanisaidia kujiunga nao.ningependa kuwa nanunua bidhaa kwa ajili ya nyumbani kwangu hasa sabuni ya kufulia.nitashukuru sana kwa msaada wako.
  stay blessed.

  ReplyDelete
 2. Hi sylvia.Nimefurahi kusikia wall papers zinapatikana kwako. Zinagarimu sh ngapi kwa sequare meter (Kununua karatasi na kubandika)?

  ReplyDelete
 3. hi, wallpapers zinagharimu 30,000/- kwa square meters. na hii ni pamoja na kubandika kabisa.....karibu

  ReplyDelete
 4. hey dada wow je hizo ni za wapiii china auu uk unaranfi za plain naweza bandika chooni

  ReplyDelete
 5. Hi Sylvia mimi ni solomon,blog yako imenikumbusha mbali sana kijijini tangu nikiwa mtoto mdogo, niliwasikia wazazi wakisema tunaenda sokoni kununua KISADO cha mahindi, KISADO cha nyanya, duuh!! kumbe neno KISADO limetokana na neno SADOLIN kampuni ya rangi madhubuti tangu enzi za mababu zetu. RANGI ambazo ukipaka kwenye nyumba yako zinadumu hadi watoto wanafikia umri wa kuoa na kuolewa! Na sasa unasema wamekuja na RANGI za DULUX, HEEEH! kweli SADO ni kiboko, wametukomboa sisi wenye vipato vya chini tusiotaka kurudiarudia kupaka nyumba RANGI kila mara,unapaka mara moja tu! unasahau.

  ReplyDelete
 6. Je hizo wallpaper haziharibu ukuta utakapozitoa?

  ReplyDelete