Friday, November 30, 2012

Stoo za jikoni.....

Leo naomba tuangalie upande wa stoo zetu za jikoni, mpangilio ukoje? usafi je? shelf nazo zina hali gani.....ama kama hauna shelf ufanyaje?

Tumekua tukijisahau kwa upande wa stoo za jikoni, na mpangilio sio mzuri.....kumbuka stoo hii mara nyingi mahali hapa ni pakuwekea akiba ya chakula.....sasa kunatakiwa kuwe kusafi muda wote, maana ukipaacha ndio panakua ni chanzo cha panya, mende etc...kuweko mahala hapa....

Nimeweka baadhi ya picha ya jinsi unatakavyoweza kuweka mpangilio mzuri wa stoo yako...iwe kubwa ama ndogo... zote zinatakiwa kua katika hali nzuri na kuwafi muda wote....






 Kama tunavyoona mpangilio, unatakiwa kuweka vyakula kwenye makopo yanayoonyesha ndani, kama ni ya glass ama plastic na kama hauna basi weka lebo ili utakapo kua unataka kutumia basi iwe ni rahisi kujua nini uchukue na urudishe kiurahisi
 Inategemea na stoo yako imekaaje...kama ni ndogo basi tengeneza shelf kulingana na ukubwa wa stoo. kama hii inayoonekana hapa ni ndogo...




 Kwa mpangilio wa vitu, vitu vizito siku zote vinatakiwa vikae chini, nikimanisha ndoo za mafuta, madumu etc.... na usichanganye chakula na vitu visivyo ni chakula.....









Baadhi ya design za stoo.....najua mpaka hapa utakua umepata wazo la vipi utengeneze stoo yako ama ui karabati etc...

Nawatakia weekend njema......

No comments:

Post a Comment