Monday, November 26, 2012

Site ya Kigamboni.....Homez Deco tuliweka Kabati la nguo la Mninga....

 Hili ndilo kabati languo la mninga muonekano wake wa nje.....mteja alihitaji kabati litakaloweza kuhifadhi nguo za watoto wa kike wa wili na kama atatokea mgeni basi nae anaweza akaweka nguo zake hapo....na wote waweze kuweka viatu....
 Kabati muonekano wa ndani.....Kama unavyoona Kushoto na kulia kuna fanana, nikiwa na maana ya kwamba, kuna sehemu ya ku hang nguo, kuna sehemu ya ku kuweka nguo zilizokunjwa, na kuna droo mbili kila upande, na katikati ndio sehemu ambapo mgeni akija basi ana uwezo wa kuweka nguo hapo bila kusumbua wengine.....na chini ndio sehemu ya kuweka viatu....
 Kama kawaida, nikiwa nimepozi mbele ya kazi yangu baada ya kuikagua na kuridhika nayo....

NB:
Mbao nzuri kwa makabati ni mninga, mkongo, kwa wale wanaojiweza...na kuna mbao zingine ambazo ni mpodo, etc.....Mbao ni gharama hasa kwa kipindi hiki ambacho miti haikatwi katwi ovyo.....

Mninga ama Mkongo, ni imara na hupendeza sana.....

Waweza pia kutengeneza kabati la nguo la MDF, ni haya makabati ya ready made.....ambayo tunayaona madukani....ila sio imara kwakweli, na hayataki shida, kama kuhama hama, etc...

Karibuni sana kwa mahitaji ya makabati ya nguo, ya jikoni, etc.....

Homez Deco tutakuja kupima nyumbani kwako ama sehemu utakayotaka tukuwekee...maana hatupokei vipimo vya mteja.....na kukupa bei kulingana na design, na mbao uliyoichagua.....

1 comment:

  1. ningependa kujua kama unafanya kama dalali au ni wewe ndo una hao mafundi wa furniture. i mean unalipwa consultation au na furniture

    ReplyDelete