Friday, January 29, 2010

Grocery Shopping List


Nimesoma maoni yenu, na mmejitahidi kunisaidia kuelimisha jamiii, ni kweli kabla huja kwenda kununua vitu vilivyoisha ni lazima ufanye stock taking ujue ni vipi vipo na vipi vimekwisha, na hii itakusaidia kununua vitu kwa budget pia. Mtakubaliana nami kuwa kadri siku zinavyokwenda ndivyo unavyotakiwa kufanya vitu kwa budget.

Hii itakusaidia sana kununua vitu ambavyo sio vya muhimu kwa muda huo, na pia utakuwa unaweza kuwa na akiba kwenye account yako.

Hii ni list ya kujaza kabla ya kwenda kununua, itawasaidia sana na haitakupotezea muda kwani ukisha ijaza utajua ni wapi kitu fulani kinapatikana wapi, hivyo utaokoa pesa na muda pia.

Nawashukuru wote kwa kuchangia mada.( Kwa mtakao hitaji list hii pls nitumieni email address zenu nami nitawatumia list hii. Itawasaidia sana)

No comments:

Post a Comment