Wednesday, January 20, 2010

Ni kujipanga tuuu na kila kitu kitaenda sawa!!!

Nimekuwa nikipata maswali mengi sana, kuwa ninajigawaje muda wangu na mpaka nimeweza kufika hapa nilipo? Ni swali rahisi lakini ni gumu kidogo.

Sasa basi mimi ni mfanyakazi wa kampuni moja hapa mjini (jina kapuni maswali sitaki), Huwa ninaingia kazini saa mbili kamili mpaka saa kumi na moja jioni.

Ninapoingia huwa niko serious na kazi za mwajiri wangu, na huwa ninajitahidi kuwahi ili ni update blogsite yangu hii, kabla muda wa kuwa busy hapa ofisini haujaanza. Namshukuru mungu kwa hili kwamba linafanikiwa.

Baada ya hapo huwa ninaendelea na kazi na kama simu za wateja zinaingia huwa napokea nakwenda visitors room naongea nikimaliza narudi mzigoni, Kama nina order za wateja za mapazia, cusion covers, pillow cases etc, huwa ninatumia muda wa lunch maana tunapewa 1hr, kutafuta materials, then narudi ofisini.

Jioni nikitoka kazini ninapitia dukani mpaka usiku kwenye saa mbili ndio nitoke ila kuna kuwaga na wakati mwingine huwa na kazi ya kufunga curtain poles kwa watejahizo hata katikati ya week huwa nakwenda na mafundi wangu.

Weekends, huwa unakuwa ni muda wa kuonana na wateja wangu, sasa hapo ndio kama kuna wa kwenda kuwaona majumbani kwao, etc, na huwa nina charge tshs. 15,000/- kwa kwenda kwao. Huwezi amini wengi wao huwa wanalalamika eti ni kubwa. Hivi kweli unaweza kwenda kwa mteja, ukampimia kazi yake, halafu hata hela ya mafuta basi, na muda, uliotumia kwenda - hakuna? Inawezekana?

Ninapenda kuchukua fursa hii kumshukuru Darling wangu kwa surport anayonipa na uelewa wake wa kunielewa, na huwa ninakwenda nae kwa wateja kwenda kufanya kazi za wateja. Mafanikio niliyonayo mpaka sasa yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na yeye, hunifariji ninapokuwa na stress za mafundi, wateja wenyewe etc. YOU KNOW WHO U ARE, I LOVE U WITH ALL MY HEART, AND THANK U SO MUCH FOR ALL THE COMFORT, LOVING, SHARING, SUPPORT, ETC, WHICH YOU ARE GIVING TO ME.

Kwa kusema ukweli huwa ninachoka sana, ila ndio hivyo, kazi hii ya interior designing ninaipenda kutoka moyoni, na ndio maana ninaifanya kwa moyo wangu wote. Huwa ikitokea mteja hajaridhika na kazi aliyonipa huwa roho inaniuma sana na niko radhi kuirudia kazi ile bila yeye kutoa hela yake, ila kama kosa liko upande wetu.

Nawashukuru wote kwa support mnayonipa. MUNGU AWE NANYI KATIKA KUJENGA TAIFA HILI LETU.

1 comment:

  1. safi sana. Hiyo itakusaidia kuepukana na mambo mengi yasiyofaa katika jamii. Na hapo kuna wale wenye wivu wataanza kusema unajidai huna muda wa kuwa nao wakati wewe unatafuta hela. Napenda unavyojituma. Endelea hivyo hivyo mdogo wangu

    ReplyDelete