Wednesday, January 20, 2010

HII NI BEDROOM MTOTO AU WATOTO WA KIUME(Imeletwa kwenu na Mrs. Jossanne)



Naomba wasomaji wetu mzingatie mpangilio mzima wa rangi kuanzia kenye kuta za chumba kitanda ila silazima uwe na rangi uwe na rangi za hicho kitanda unaweza kuchongesha au kununua plain colors or just pine woods, bed, inategemea na uwezo wako ila kwa ushauri tu, zingaiti rangi za majumbanikwetu nimeona watu wengi napenda dark colors dark pink dark red, oranges jamani hizi rangi azifai kwa DAR. maana weather ya dar ni joto pia rangi zina giza iwe chumbani au living room jikoni, kwa watu wa DAR, umejenga hse yako au umenunua piga cool colors, soothing colors ambazo zinafanya nyumba iwe na mwanga wa ktosha, achaneni na dark colors ndio maana kuna washauri wakina home deco nenda upewe ushauri, unaweza kuwa na pesa ila una ideal ya baadhi ya vitu sehemu za biashara zina rangi, shule maofisini majumbani, saloons, madukani kila sehemu kuna rangi special za kupendezesaha ila tuachana na marangi yanoyowaka shouting colors is BIG NO KWA DAR.

(From Sylvia - Nakushukuru sana Dada Jossanne kwa makala zako za mara kwa mara za kutuelimisha, kwa kweli hapa Tanzania tuko nyuma sana, na wengi wetu tumekuwa tukidhani ya kuwa tunajua lakini hatutaki kukubali kuwa hatujui, tunachofikiria ni kuwa kuliko kuita professional afanye kazi kwa umaridadi, basi tunaona tunamfaidisha huyo mtu ama utasikia ni gharama. kitu ambacho si kweli, hebu siku moja kaa na ufikiria, gharama za michango unayotoa kwenye sherehe, kununua viatu, nguo, make up, kwenda saloon , etc. Na ukiangalia nyumba unayoishi jamani inatia huruma na sio kwamba huna hela ingawa wakale walisema kupanga kuchagua, ila sio kila msemo ni wakufatwa mingine inapotosha.)

No comments:

Post a Comment