Tuesday, January 5, 2010

wapendwa wana blog ninawakaribisha tena mwaka mpya 2010 kwenye makala yetu ya utayarishaji wa bustani za maua



hizi hapo juu ni baadhi ya sehemu ambazo tulipanda.

Land scaping, au ulimiaji wa bustani za maua, miti majani mbalimbali,

Najua mikoa yetu imegawanyika, pia hali ya hewa ni tofauti, kuna sehemu mvua zimeanza kunyesha, au zitaanza karibuni.

Kwa hiyo ambao mnajua msimu wa mvua unaanza karibuni mnaweza kuuanza kupanda maua, au miti inayoweza stahimili, maji na ambayo itahifadhi, maji kwa muda.

Jua litakapoanza kuwa kali najuwa kwa DAR. ndio kunaanza anza mvua za hapa na pale. Tayarisheni bustani zenu kufuatana, na msimu, ikiwa ni msimu wa mvua mpaka masika pandeni miti, tunaelewa umuhimu wa miti, karibu na nyumba, majengo, au mashuleni.

Wale ambao wako mikoa yenye baridi kari kama ARUSHA, IRINGA, sio msimu wa kupanda chochote, subirini mpaka mvua zianze ili ardhi iwe imepoa na baridi maana maua mengine miti, au majani huwa hayaoti wakati wa baridi, ila unaweza kuanza matayarisho kulimia kuweka mbolea, pia ninawashauri tumieni mbolea itokanayo na mifugo ni nzuri, haina side effects au madhara.

Pia angalia eneo unalotaka, kuweka bustani, au kupanda miti lazima ujue hiyo miti inakuwa kwa urefu gani?? na kwa muda gani siwashauri kabisa, kupanda mianzi au bamboo ni miti ambayo ina madhara sana, mizizi yake inaenda eneo zima pia inauwa mimea mingine ambayo iko karibu


Ndio maana mnaonaga siku zote inaota kwenye mito au kwenye kingo ziwa pia inaitaji maji mengi, siwashauri kupanda mianzi nawatakia undaaji mzuri wa bustani zenu

Miti , maua majani hata sisi Tanzania tunaweza kubadilisha, nchi yetu, miji tunayoishi, mitaa ikawa kama kwa wenzetu tushirikiane kuanzia ngazi za familia hadi taifa naamini kabisa, penye nia pana njia. nawatakia mafanikio ktk kazi zenu asanteni,

JOSSYANNE GEORGE.NEW YORK.

No comments:

Post a Comment