Thursday, January 28, 2010

Wanawake wenzangu tutapona kweli????

Leo asubuhi wakati niko njiani kuja ofisini kwenye gari, nilikuwa ninasikiliza kipindi cha power breakfast, na huwa ninakisikiliza kila siku.

Ilipofika saa moja kamili, ilikuwa ni muda wa taarifa ya habari, nikasikiliza weeee kama kawaida yangu, jamani nilisikia kuwa kuna pedi za always feki. Lol moyo ulifanya paaahhhhh.

Habari ilisomwa hivi..... najitahidi kunukuuuuu

Jangwani, kulikuwa na malori yanashusha mizigo kutoka kwenye lori na kuingiza kwenye gari lingine, ila kulikuwa na watu na waliwastukia na kutoa taarifa polisi.

Polisi walipofika pale waliuliza mwenye mali na akatokea muhindi na walipokagua mzigo wakakuta ni ALWAYS FEKI, muhindi akaulizwa kazitoa wapi akasema kanunua kwa ajenti Arusha.

Walipofuatilia ajenti huyo hawakumkuta, alikimbia, na wakaangalia kwenye ghala wakakuta pedi 8,000 aina ya always na zote ni feki.

Jamani wanawake wenzangu tutapona kweli???????????????????

No comments:

Post a Comment