Tuesday, October 1, 2013

MAANDALIZI YA MWISHO WA MWAKA KATIKA NYUMBA ZETU.......

Wengi wetu tumekua na kawaida ya kujiandaa kwa ajili ya mwisho wa mwaka, kama kwenye maofisi basi tunapamba ofisi zetu kwa mapambo, na kama ni kwenye nyumba zetu basi nako tunajiandaa kufanya maandalizi.

Asilimia kubwa kati yetu ni kua hua katika kipindi hiki hua tunajitahidi kumalizia nyumba tunazojenga ili tunahamia, na wengine tunahamia kwenye nyumba zengine za kupanga....kubadilisha mazingira....etc.

Katika yote haya maandalizi yanahitajika.......na inategemea pia na nyumba yenyewe inahitaji nini.....

Kwenye upande wa matengenezo, ama rangi, etc....

Bila kusahau pia fanicha, nazo pia inatubidi tuangalie, kama zinahitaji marekebisho, ama zinahitaji kubadilishwa kabisaaa.....yote haya yanaanzia kwako na wewe mwenyewe.

Katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ndio wengi wetu tanaangalia je yale malengo yetu tuliyoyapanga kwa mwaka mzima yamefanikiwa, ama yalikaribia kufanikiwa.

Napenda kukumbushia kua hiki ndio kipindi cha kufanya maandalizi ya nyumba zetu......kwa usafi, kutoa vitu ambavyo hauvihitaji na kugawa, na kama kuna vitu vibovu basi ndio wakati wake wa kuviteketeza.....

Pale ambapo unapopanga mikakati yako ya kimaendeleo, tusisahau na nyumba zetu.....

Jamani nyumba nazo zinahitaji service.....yaweza kua ni ya kila mwaka, ama ya baada ya miaka kadhaaa....ni wewe mwenyewe ndio utaangalia nyumba yako iko katika hali gani.....

Tumekua tukijisahau sana kwa upande wa kufanyia service nyumba zetu.......na mwisho wa siku unakuja kukuta matengenezo yanakua ni gharama zaidi ya matarajio yako..........wakati ungekua unafanya service ungeepuka tatizo hili la gharama mara dufu......



No comments:

Post a Comment