Wednesday, November 13, 2013

FINNISHING YA NYUMBA ZETU........Wengi wetu tumekua tukidhani kua kazi nzito ni ujenzi wa nyumba na sio finnishing,,,,naomba kuwaeleza leo kua sio kweli kwa asilimia flani........

Jamani finnishing ya nyumba ni gharama kuliko ujenzi....tutambue hilo, na utakuta wengine mpaka miaka kadhaa hawajamaliza, kwa kua wanajua nini wanafanya ...

Kinachohitajika ni kujipanga, na kutafuta mtaalam aweze kukusaidia katika hili....unaweza kujenga nyumba yako vizuri...lakini ukija kwenye finnishing unaanza kubania hela na kutaka virahisi...yaani jua kua nyumba unaiharibu na hutokua umefanya kazi yoyote ile......nyumba itakua mbaya mbaya na unaweza kujuta.....


Tujitahidi katika hili kua kama najenga nyumba yangu basi ni afadhali nifanye taratibu kwa ufasaha kuliko haaraka haraka na ukaharibu kazi......

Tujitahidi kua wavumilivu katika kumaliza nyumba zetu kuliko haraka haraka, ninasema hivyo kwa kua nakutana na watu kama hawa, na kwa kweli katika kazi yangu sipendi haraka ya kupitiliza kabisaaaaa.......

Kazi ya designing inahitaji muda na nafasi. bila hivyo ni kuharibu kazi.....nami sipendi hilo litokeeee....

Kwa kwetu Tanzania bado tuko nyuma katika hili ingawa tunajikongoja na tutafika kwa kuelimishana na kuelewana...
Sasa hivi vifaa ama vitu vinapanda bei kila kukicha na viko vingi mno ni wewe mwenyewe kuchagua nini unataka na nicha cha wapi kitumike....

Sababu ingine utakuta unamwambia mteja kua hapa panahitajika hiki na hiki, halafu mteja anakua mbishi....oooohhhh hela nyingi mara sababu hiiiikatoa....sasa jamani unavyokataaa fundi afanyaje? na nyumba ikiharibika utamlalamikia fundi sio......unasahau kua ulikua mbishi.......

Mara nyingi mafundi wazoefu wanajua kipi kizuri na kipi kibaya, yaani kama wewe ulivyo kazini unajua kipi kizuri na kipi kibaya. Sasa usiposikiliza ushauri na kutaka ufanyavyo kazi ikiharibika usilalamike.....

Napenda kutumia msemo huu: RAHISI GHARAMA......

Asilimia kubwa kati yetu hua tunapenda vitu vingi rahisi kuliko vitu vichache vinavyodumu na vizuri.....(ntakuja kuliongelea siku ingine)

Homez Deco kwa kweli hatufanyi kazi ili mradi kazi iishe tuchukue hela........tunatoa ushauri kwa mteja.kwanza  na kama   anataka ilimradi iishe basi hua kazi hatufanyi, maana mwisho wa siku ni kuharibu jina letu, na muda wetu.....

Inafika mahali tuambizane ukweli sasa.....

Kitu kingine nilitaka kusahau, jamani baadhi yetu tumekua tukiwabana sana mafundi katika malipo, kitu ambacho si haki hata kidogo, na ndio maana utakuta mafundi wengine wanakuachia kazi, ama wanafanya vibaya kuharibu....etc.   Nashauri tuelewane na mafundi kwa kazi utakayompa na mkubaliane.. na akimaliza kazi yake basi mmalizie hela yake....wateja wengine hata kumalizia hela ya fundi inakua tabu na kazi keshafanya......(ni malalamiko ya mafundi baadhi nilioongea nao)


Naomba tubadilike na tutengeneze nyumba zetu vizuri na ziwe zinavutia na kutazamika na utakaa kwa amani, hutokua na kurudia rudia mara kwa mara.....ni kupoteza hela ambapo ungeitumia kwa vitu vingine.


No comments:

Post a Comment