Tuesday, September 4, 2012

Ubatizo wa Jaydan, ilikua ni tarehe 1/9/2012

 Jaydan akiingia kanisani na dada yake
 Tuko kanisani tayari na Jossyanne ndie mama wa ubatizo wa Jaydan

 Jaydan akibatizwa akiwa ameshikwa na mama yake wa ubatizo.....kwa kweli machozi yalinilenga lenga kwa furaha.......
 Kwa sisi wa kristo tunakua na kitu kimoja kwamba ukizaa nje ya ndoa basi unatengwa, sasa unahitajika kurudi kanisani na utubu dhambi zako, na hapa ndicho kilichokua kikifanyika.....

 Nilipewa mtoto wangu baada ya kurudishwa kanisani, na tuliombewa.... yaani nilijihisi nimetua mzigo maana kifua kilibaki chepesi sna..... namshukuru mungu kwa kila jambo analonitendea na mwanangu.....mungu ni mwema
 Jaydan baada ya kubatizwa......nakupenda sana mwanangu kuliko kitu chochote hapa duniani....tuna mwaka na miez sita sasa....
 familia... akiwa na bibi na shangazi
 Hapa Jaydan akiwa na bibi yake mzaa mama  na mama yake...
 Jaydan na mama wa ubatizo na mie nina mtoto wa ubatizo jina lake ni Samantha ana miezi 5....nina watoto 2 sasa... nawapenda wote
 Tukiwa na mtoto wetu wa ubatizo Samantha, huyu ni kaka yangu.....
 Jaydan na bibi na mama
 Haya huyu ndie baba wa ubatizo wa Jaydan ni mdogo wangu
 Na huyu ndie mama wa ubatizo Jossyanne. wengi wenu mwamjua....love u sis....n anakushukuru kwa kua nasi siku hiii....
 Mama mzaa chema.... hahahhaha
 Jaydan katika pozi.....
 Kwa kweli nina kila sababu ya kumshukuru dada anaekaa na Jaydan, maana sijui ingekuaje, kwa kazi ninazozifanya narudi usiku, nimechoka, na namkuta Jaydan hana tatizo lolote kwa kweli. nakushukuru dada Jaydan. Ninae tokea nimejifungua Jaydan....
Familia baada ya kutoka kanisani...... nawapenda wote.....

NB:
Ubatizo ulikua wa kimya kimya jamani samahani sana kwa kua mchoyo kuwakaribisha.....nawapenda wadau wangu woteee

8 comments:

 1. Hongera sana dear kwa kubatiza na kurudi kundini. MUNGU wetu ni mwema sana, akulinde wewe na Jaydan.

  ReplyDelete
 2. ongera mamy!Mungu ni mwema ck zote

  ReplyDelete
 3. Hongera sana mama Jaydan, yani mmependeza mnoooo, i love your shoes. Nimefurahi hadi nimeskia kulia na mimi, jaydan is soo sweet, Mungu akukuzie na kuzidi kukupigania.

  Mama yako kijana kweli, kama dada yako, mpe bigup kwa kujkeep vzr.

  Mteja wako

  ReplyDelete
 4. Hongera sana mamie kwa kurudi kundini. Na hongera sana kwa kubatiza mtoto. Mwenyezi Mungu akukuzie jaman. So nice

  ReplyDelete
 5. Jaydan keshakua mbaba mzima hongera sana na ubatizo, mama mzaa chema umetokelezea howt kiatu dear umefunika look yote pendeza sana, familia yako imetulia mbarikiwe sana. Jaydan kafanana sana na bibi yake, mama wa ubatizo hongera uko nyumbani likizo? karibu

  ReplyDelete
 6. safi sana sylivia kuna mtu alicomment humu ujinga alinikera sana, ila mungu ni mwema umeweza kumbatiza mtoto wako na umerudi kundini mungu aendelee kukusimamia siku zote za maisha yako, na akukuzie mwanao, single parent pia wanaweza kulea watoto wao bila tegemezi yoyote keep it up dear

  ReplyDelete
 7. hongera dear, Mungu ni mwema na kwa kurudi kundini Mungu azidi kukutunza wewe na mwanao. aibariki familia yako kwa kua nawe wakati wote.

  ReplyDelete
 8. nimependa,hizi ndo huruma na msahama wa Mungu wetu kwa sie binadamu kwani bila yeye hatuwezi,Mungu wetu hatuhukumu bali utusamehe yote!nimependa jumbe zako
  zaidi nimeguswa sana na dada anaekulelea mtoto jinsi ulivomshukuru inaonekana ni kati ya wadada wanaoishi na mabosi zao vizuri na kutunza watoto bila shida...nimepmenda dada yako!!

  ReplyDelete