Tuesday, September 11, 2012

Open Kitchen

 Mbao...
Mdf
 Mbao...
 Mbao....
 Mdf
Mbao..

Hizi ni baadhi ya majiko ya wazi, ambayo leo nimeona nizungumzie.

Hapa kwetu Tanzania, naona sasa hivi ndio kidogo watu wameanza kua na majiko ya aina hii, ambayo ukikaa dinning ama livingroom basi unaliona jiko lako na kila kitu kilichopo ndani....

Aina ya majiko haya ni mazuri sana, na haijalishi, udogo wa eneo ama ukubwa wa eneo...... kote yanapendeza kulingana na utakavyopangilia.....

Kwa upande wa aina ipi utumie, inategemea na uwezo wako, unaweza kutumia mbao, mninga, mkongo, makabati yaliyo ready made..... yote yanapendeza...

Aina hii ya jiko linahitaji usafi wa hali ya juu mnooo....na kama uko na mwenzio ni vizuri mkashauriana kwanza na mkakubaliana ndio muwe nalo,

Jiko la aina hii linatakiwa saa zote liwe safi, vyombo viwe visafi, na hata mpikaji awe ni msafi, na dasta anazozitumia ziwe safi.... bila ya hivyo itakua ni matatizo tuuuu....

Jiko hili halitaki kujaza vitu, yaani vyombo, ama vitu vikawa viwili viwili........

Nawashauri kwa wale watakaotaka kua na majiko ya aina hii kwa nza wafikirie mara mbili  mbili kabla ya kuwa nalo.....

No comments:

Post a Comment