Thursday, September 27, 2012

Ungependa kuuza fanicha ulizonazo.......Karibu utangaze nasi, kwa mahitaji ya kuuza fanicha ulizonazo, itakusaidia uweze kupata hela ya kuongezea na kununua ukipendacho...

Naomba kwa atakayependa anitumie picha kwa email na kuweka namba zake za simu ama ni jinsi gani atapatikana....

Kuna gharama kiasi ya kutangaza kwa mwezi mzima.....

Homez Deco, HAITAHUSIKA KWENYE UUZAJI AMA UNUNUZI KATI YA MUUZAJI NA MNUNUZI........

Homez Deco tumeona tufanye hivi kwani itakusaidia sana, kupunguza vitu ulivyonavyo, na kupunguza mlundikano wa vitu nyumbani kwako. Kuna baadhi ya watu ambao hawawezi kugawa vitu, kwa ndugu ama marafiki, na wamevifungia tuu stoo. ama kuwa na mlundikano tuuu ndani......

Imefika wakati sasa tupunguze vitu majumbani mwetu kwa kuweza kupata muonekano mzuri na wakisasa...

Vitu mtakavyoviuza, naomba viwe katika hali nzuri, kwani pia nitachagua kabla ya kuvirusha kwenye blog.

Upige picha pande zote ili tuweze kuona....

Vitu hivi vya kuuza vyaweza kua ni fridge, tv, jiko, makabati, vitanda, sofa, meza za chakula na vinginevyo ambavyo wewe mwenyewe unaona kabisaaa, sasa ninaweza kuuza, ili nipate nafasi, ama ununue kingine......

NB:

Tafadhali tunaomba vitu hivi viwe katika hali nzuri.......karibuni nyote.... Sylvia - Homez Deco

No comments:

Post a Comment