Monday, August 27, 2012

Mapambo ya Kiafrika

 Nimeombwa kuonyesha mapambo ya kiafrika na ninapenda kujibu maombi yenu, katika picha hii hapo juu, hapa kitenge kimetumika katika mito na sofa< na kama inavyoonekama imependeza vizuri tuuu, sasa kwa wewe unayependa mapambo ya kiafrika, unaweza ukabadilisha sofa lako kwa kutumia kitenge ama batiki na ikapendeza tuu, ila uwe mwangalifu na rangi, maana vingine hua vinachuja....
 Hapa napo ni aina ya vitenge vya west africa kama sijakosea, mtanisahihisha.... na ngozi hii ya punda milia inatumika kama decorative carpet.....
 Vitenga havijaachwa nyuma,,, na ngozi ya ng'ombe hiyo hutumika kama decorative carpet
 vitambaa vyenye picha za aina ya tingatinga nazo ni nzuri kwa kutumia.....


Ninachoweza kusema ni kua kwa kutumia vitenge, batiki, ngozi za wanyama, vibuyu, na vitu vyote vya kiafrika katika nyumba yako kwa wale wanaotaka kua na mandhali ya kiafrika, inawezekana, na vitu hivi vinapatikana hapa hapa kwetu Tanzania.

Kwa hapa Dar unaweza kuvipata Mwengem Sleep way, na kwenye hotels.... naomba kwa wale wa mikoani mnisaidie wapi tunaweza kupata vitu hivi ili tuwajulishe wenzetu wapi wanaweza kupata kwenye mikoa yako kwa urahisi...

nitumie sms kwa kupitia 0715 - 920 565 na nitaleta humu humu kuwaelekeza........

No comments:

Post a Comment