Wednesday, September 19, 2012

Rangi zinazoshauriwa kutumika vyumbani.....




Nadhani kila mmoja wetu anajua vyumbani ni sehemu ya kulala, iwe ni mchana umejitupa, ama usiku unalala, maisha yetu siku zote yanahitaji mwili upumzike baada ya kazi ya siku nzima......haijalishi ni kazi gani...

Sasa basi kwenye vyumba vyetu, kwa upande wa rangi, kuanzia ukutani, mashuka, pazia etc. ningependa kushauri kua tusitumie rangi kali sana tena hasa kwenye upande wa ukutani, maana ukutani mpaka uje kubadilisha rangi na hatuna uratibu wa kubadilisha rangi mara kwa mara basi paka rangi ambazo zimepoa.

Rangi ambazo zimepoa ni kama hizo hapo juu, rangi hizi zinasaidia sana hasa katika maisha yetu....

Hivi umeshajiuliza kwanini ukiingia chumbani kwako maraa baada ya muda kidogo kichwa kinakuuma, mara kwa mara, ama macho etc..... sasa hebu angalia chumbani kwako kama rangi uliyoipaka ukutani ni kali sana....ama la....lakini kama umepaka rangi tuuu zilizopoa basi tatizo hilo litakua ni la kiafya zaidi....

Ningependa kushauri kwa wale wanaopenda kupaka rangi kali vyumbani, wasipake, na badala yake wapake rangi hiyo hiyo ikiwa imepoa zaidi.......kama picha zetu zinavyotuonyesha hapo juu....

1 comment:

  1. ni kweli my dia. nimependa kila kitu hapa.

    ReplyDelete