Monday, August 31, 2009

Tunaongea na mifano ama sivyo?





Jinsi ya kuning'iniza picha za ukutani

Picha za ukutani ziko za aina nyingi sana, na wengi wetu tunapenda sana picha mie mmoja wapo. ila wengi wetu hatujui jinsi ya kuzi ning'iniza picha hizo kwani utakuta ukuta una matundu matundu ya misumari ndio ujue hapo kazi ya picha ilikuwako.

Kuna step 4 za kufuatwa kabla ya kuning'iniza hizo picha na haijalishi ni picha gani wadau wangu. Vitu vinavyohitajika ni:

  1. Penseli
  2. Karatasi
  3. Nyundo, drill
  4. Misumari ama hook za ukutani

Steps:

  1. Kwanza angalia ukuta wako ni wa aina gani ili ujue kama utatumia grill ama nyundo, halafu chagua ni sehemu gani ya ukuta unataka kutundika picha zako, Picha kubwa huonekana vizuri kwenye ukuta mkubwa(sehemu ya ukuta pawe pakubwa), na picha ndogo huonekana vizuri kwenye ukuta mdogo na ni vizuri ziwe picha mbili mpaka tatu yategemea na sehemu ya ukuta wako. ( sehemu ya ukuta pawe padogo) 
  2. Hakikisha una ning'iniza picha zako usawa wa macho, isiwe juu ama chini. Picha kubwa zaidi hupendezea kutundikwa juu ya sofa ama sehemu ya kuwashia moto sitting room kwa wenzetu walio sehemu za baridi.
  3. Chagua picha unazotaka kuzining'iniza ni vizuri ukizichagulia sakafuni, halafu kata karatasi usawa na hizo picha, chukua penseli yako na hiyo karatasi nenda ukutani jaribishia ukiona iko sawa basi weka alama na penseli yako, chukua hook ama misumari pigilia tayari kwa kuning'iniza picha zako.
  4. Kuning'iniza picha za group, zisambaze sakafuni, chagua na jaribu kuzipanga kubwa kwa ndogo ama ndogo zote na angalia ukiona umeridhika na muonekano wa picha hizo, basi fuata stepu hizo 3,kwa wale wenye nyumba za ghorofa tundika kwenye ngazi, pia yapendeza. Na utakuwa umependezesha nyumba yako na HAKUTA KUWA NA MASHIMO MASHIMO.

Maana ya pisi za maua waridi (rose)

Pisi 50 - Mapenzi yangu kwako hayana kikomo
Pisi 24 - Mimi ni wako
Pisi 12 - Kuwa wangu
Pisi 6 - Nimeanza kukupenda
Pisi 3 - Wewe, mimi, na penzi letu kwa pamoja
Pisi 2 - Naomba tuwe pamoja
Ua 1 - Nakupenda na wewe ndio chaguo langu

Thursday, August 27, 2009

Vyoo vyetu

Kuna mdau kaniuliza swali kuwa, hicho pembeni ya choo chenye bomba ni kwa ajili ya nini? Jibu ni kwamba hilo ni sinki ya kutawazia kwa wale wasiotumia toilet paper.

Henga za bafuni

Kuna mdau kaniuliza kama zaweza patikani hizi henga, jibu ni kwamba zinapatikana nitajitahidi kuleta aina tofauti ili muweze kuchagua.

Mhhh hii kali, ni mito jamani lol!!!!




Henga za bafuni

Style zaidi .......

Maana ya rangi za mishumaa

Kijani: Kutengwa, kukua, hela, mafanikio, utajiri, uponyaji wa mwili, ndoa, uzazi, kazi, balansi, kichochezi cha ukuaji, mafanikio ya kifedha, kutakiana kheri, kazi mpya, mavuno mazuri, love etc.

Njano: Busara na heshima, vitendo, kuvutiwa na ubunifu, kusoma, uwezo wa akili, umakinifu, kumbukumbu, mvuto, kujiamini, furaha, mabadiliko, usalama ect.

Nyekundu: Nguvu, mapenzi, ulinzi, upendo, moto, uzazi, upendo wa mwili na matamanio, kujipa moyo, mvuto, uhitaji, etc.

Nyeupe: Ulinganifu wa rangi zote, mwangaza wa kiroho, usafi, uponyaji, utafutaji wa ukweli, kutokuwa na hatia, umoja, amani, ukweli, ulinzi, uponyaji wa hisia, huondoa mtazamo hasi etc.

Pinki: Upendo, urafiki, mapenzi, heshima, ukaribu, kukaribisha ushirikiano, upendo usiokuwa na kikomo, umakinifu, rangi ya kike etc.

Dhahabu: Mwangaza, ulinzi, mafanikio, utajiri, hela, uanaume, mgawanyo, ushindi, bahati etc.

Lavender: Hali ya kiroho, uchangamfu, kuvutia usaidizi wa kiroho, uwelewa, usaidizi, udhihirisho na kutokuwa na ubinafsi etc.

Bluu: Mawasiliano, ukweli, amani,utulivu, uelewa, busara, ulinzi, uvumilivu, furaha, afya, utiifu etc

Rangi ya Chungwa: Mafanikio, malengo, mvuto wa vitu vizuri, husafisha mtazamo hasi, tukio na mahali, makubaliano ya kibiashara, mabadiliko ya ghafla, nguvu, kuvuta mafanikio, inavuta marafiki, inatia moyo etc.

Brauni: Kukuza mafanikio ya kifedha, ulinganifu wa rangi, inasaidia kutafuta vilivyopotea, nyumba, maajabu ya wanyama, urafiki, maajabu ya dunia, etc.

Papo: Inatumika na rangi nyeupe kupunguza ung'aavu, meditation, kujiamini, maarifa yaliyofichika, ukuzaji wa ulichonacho, kutambulika kazini etc.

Waridi: Kuona huruma kwa mwenyewe na wenzako, nguvu, moyo mkunjufu, msamaha, ubunifu, uvumilivu, mapenzi, uponyaji, etc.

Peach: urejeshwaji etc.

Violet: Nguvu, mafanikio, ubunifu, uhuru na mafanikio ya kifedha na uanzishwaji wa mahusiano mapya na wengine, 

Ivory: Ulinganifu, usiokuwa na madhara, kawaida etc. 

Nyeusi: Ulinzi, kuharibu uovu, etc.  

Silva: Uondoaji wa nguvu hasi, ushindi, uthabiti, kuondoa, etc.

 

Maana ya rangi za Mishumaa


Wote tunaijua mishumaa, iko ya aina tofauti tofauti inayotoa marashi na ambayo haitoi. Na kuna inayodondosha maji na isiyodondosha maji.

Mishumaa hutumika kama mapambo majumbani, hutumika pia gizani,  sherehe mbalimbali na nyumba za ibada etc.

Kuna rangi mbali mbali za mishumaa, leo nimeona nielezee baadhi ya rangi hizo na maana zake.

Mishumaa hii ikitumiwa bila uangalifu hatari, yaweza kuwa chanzo cha moto.

ONYO: USIACHE MSHUMAA UNAWAKA BILA UANGALIZI, USIACHE MSHUMAA KARIBU NA WATOTO NA WANYAMA KAMA PAKA, MBWA etc. USIWASHE MSHUMAA KARIBU NA KITU KINACHOWEZA KUSHIKA MOTO KWA URAHISI. HAKIKISHA UNAWASHA MSHUMAA MAHALA AMBAPO HAPAWEZI KUSHIKA MOTO HARAKA HATA KAMA UKIISHA.

Wednesday, August 26, 2009

Vyumba zaidi

Naomba ieleweke kuwa , napenda mpate aidia ya vitu, mahali etc. Isije ikawa ndio lazima  ifanyike  kama ilivyo kwenye baadhi ya picha ninazo watumia.

Haya ni makazi ya wanyama wetu tuwapendao






Kwa wale wanaoishi na paka, nimejaribu kutatua tatizo la mahala pa kuishi na kucheza

Hizi ni baadhi ya urembo wa mapazia kwa juu





Baadhi ya Mapazia


Dizaini za Mapazia

Leo nimependelea tuongelee kuhusu mapazia. Kwenye sekta hii kidogo kuna ka ugumu kwani watu wengi huwa wanadhani ilimradi pazia tuuu. Mapazia yalianza kutumika tokea karne ya kumi na tisa. Nia ya mapazia kwanza ni kuzuia mwanga wa jua kuingia ndani, vumbi, na kuzuia watu wa nje wasione ndani wakati wa usiku na kupendezesha nyumba etc.

Mapazia yanaweza kupendezesha nyumba ama yanaweza kuharibu muonekano wa nyumba. Naomba kuwakumbusha kuwa kuna mapazia ya aina 2. Mepesi na Mazito. Muangalie na Texture ya mapazia.

Mapazia yako yaliyotengenezwa kabisa na kuna ya kuchagua kitambaa kikashonwa.

Sehemu za baridi ni vizuri kuweka mapazia mazito na za joto weka mepesi. Nikisema mepesi sio yale ya kuanganza ndani bali vitambaa vyake vinakuwa sio vizito sana.

Kwenye dirisha kunatakiwa kuwe na mapazia mawili, jepesi linalosaidia kuzuia vumbi ndani, na la kawaida liwe zito zito kiasi kama ni kwenye joto na baridi liwe zito.

Kwa upande wa rangi ya mapazia jitahidi rangi ziwe zinashabihiana, kuna yaliyo na marembo na mengine hayana urembo wowote.

Sasa kuna dizaini nyingi sana za mapazia, yaweza kutumia katein boxi,  vimbao vidogovidogo vya curtain poles nisaidieni kiswahili, kuna ya mbao zinazofunguka, aluminium etc.

Tengeneza mapazia kutokana na dirisha lako lilivyo. Madirisha ya jikoni, stoo, ofisini na chooni ni vizuri ukaweka mapazia mafupi. Kuliko baki weka mapazia marefu na weka kambaa mahususi kwa kufungia pazia au vichuma vinavyogongewa ukutani vya kufungia wakati wa mchana.

Vipimo pia jamani vinamata hapa usiweke pazia mpaka likaburuza chini.

Kuna dizaini za mapazia ya nyumba kubwa na nyumba ndogo, msichanganye hapo maana nyumba itaonekana kituko.

Tuesday, August 25, 2009

Shukrani kwa funs wangu wooote

Napenda kuchukua fursa hiii kuwashukuru wote.  Nimekuwa nikizisoma comments zenu na nimefurahi sanaaa.

Ninachoweza kusema ni kwamba kwenye hii blog msisite kukosoa pale ambapo mnaona panahitaji marekebisho kwani mimi ni mdogo wenu,dada yenu etc, nina mapungufu pia na kwa kufanya hivyo tutasaidiana kwa kuelimishina. Hii ni blog ya kuelimishana.

Kuna mdau mmoja anasema kuwa niwe naweka vitu vya bongo zaidi, kwa hapa naomba nimwambie kuwa, blog hiii haiko kwa vitu vya kibongo tuuu bali ni vya dunia nzima, mtakubaliana na mimi kuwa tunahitaji  watu tubadilike na twende na wakati.

Na niko mbioni pia kuna ka program kanakuja kwa atakeyekuwa tayari anaweza kunipigia simu na nikaja nyumbani kwake nikapiga picha na kuziweka kwenye blog bila malipo na ni kwa Dar tuuu. (KWA ATAKAYE KUWA TAYARI).

Sio lazima kabati la vyombo liweko

wow hii pia nzuri ila sijui ndio usiwe na watoto watundu? mtanisaida kwa hili, naona huyu yeye kaweka vyombo vyote jikoni maana hana kabati la vyombo. Inawezekana

Nani kasema tuwe tunaweka meza za mbao pekee

Pako simpo na kuzuri nimependezwa nako, kuna mtaalamu yuko sinza wa kutengeneza hizi fanicha za chuma,  anapatikana sinza mori  kama unaelekea meeda ni baada ya bumzi la mwanzoni kulia kwako kuna frem zimepangana yuko hapo, nitawatafutia namba yake
Hii  iko simple na safi, hebu angalia hilo kabati wala halijaajaa vitu vingi. vyombo huwa vinakaa jikoni na kwenye hili kabati huwa vinakaa vyombo kidogo kama vya displei wajameni